Connect with us

General News

Sheria mpya ya walinzi wa kibinafsi yawaruhusu kumiliki bunduki, kuwakamata wahalifu ▷ Kenya News

Published

on


– Walinzi wa kibinafsi sasa wataruhusiwa kumiliki bunduki wanapokuwa kazini

– Vile vile, watakuwa na mamlaka ya kuwakamata washukiwa wa uhalifu ila hataruhusiwa kutumia nguvu

– Watahitajika kuwapeleka washukiwa katika kituo cha polisi baada ya kuwakamata

Walinzi wa kibinafsi humu nchini sasa wataanza kutumia bunduki na kuwakamata wahalifu kulingana na sheria mpya ambayo imetolewa na serikali

Sheria hiyo mpya pia itawaruhusu walinzi kutekeleza majukumu yaliyokuwa yakitekezwa na maafisa wa polisi hapo awali.

Habari Nyingine: Katibu mkuu wa Jubilee Raphael Tuju apuuza madai ya Ruto, kuendelea kumshauri Raila

Kulingana na taarifa aliyoitoa Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang’i, walinzi hao wataruhusiwa kuwakamata wahalifu na kuwapeleka hadi kituo cha polisi bila kujichukulia sheria mikononi mwao.

” Mlinzi wa kibinafsi hataruhusiwa kutumia nguvu anapomkamata mshukiwa yeyote wa uhalifu, atakubaliwa kutumia nguvu tu iwapo itahitajika,” Sehemu ya sheria hiyo ilisoma.

Habari Nyingine: Moses Kuria amjibu Ruto kuhusu Tuju kuwa msaliti ndani ya Jubilee

Afisa Mkuu Mtendaji wa Mamlaka ya Kusimamia Shughuli za Walinzi wa Kibinafsi Nchini (PSRA), Fazul Mohamed amezitaka kampuni zote husika kuzingatia sheria hii mpya.

Read: ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko.co.ke

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending