Connect with us

General News

Sheria za kuandaa ‘Mutura’ kubuniwa Murang’a – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Sheria za kuandaa ‘Mutura’ kubuniwa Murang’a – Taifa Leo

Sheria za kuandaa ‘Mutura’ kubuniwa Murang’a

NA MWANGI MUIRURI

IDARA ya Afya ya Umma katika Kaunti ya Murang’a, imeanzisha uchunguzi kubaini njia zinazotumika kutengeneza mutura; chakula maarufu kinachouzwa barabarani.

Mkuu wa Idara hiyo, Dkt Muthui Gitonga ameeleza kuwa uchunguzi huo umechangiwa na malalamishi ya wakazi kuhusu matayarisho yasiyopendeza kutoka kwa wauzaji kadhaa wa mutura.

“Kuna njia zilizoidhinishwa kutengeza mutura, ila tumepata habari kuwa wauzaji kadhaa hawazingatii usafi wanapoandaa chakula hiki.

Kuanzia sasa itabidi tuanzishe mikakati ya kuweka sheria za kuanda vyakula vinavyouzwa njiani,” alisema Dkt Gitonga.

Kulingana na Dkt Gitonga, walaji wa mutura wamelalamika kuwa baadhi ya wanaoandaa chakula hiki, wanatumia uchafu kutoka kwa

vichinjio kujaza mitura hiyo, licha ya kufahamu nyama hiyo haijadhibitishwa kuliwa na binadamu.

Malalamishi mengine yaliyowasilishwa kwa idara hiyo ni, kutumia maji yasiyo salama kuchemsha mutura, kutumia nyama isiyo halali, na jikoni chafu za kuandaa chakula hicho cha kitamaduni.

Mwenyekiti wa kundi la wawakilishi bunge kutoka Mlima Kenya, Bw Charles Mwangi alieleza Jumatatu kuwa, watajadili mswada wa kutengeza mwongozo wa kuandaa mutura katika bunge la kaunti, kwa juhudi za kuhakikisha chakula hicho kinaandaliwa ipasavyo.