Connect with us

General News

Spika Wetang’ula awataka wabunge wapitishe sheria ya kuweka NG-CDF katika Katiba kuzuia kesi nyingi – Taifa Leo

Published

on

Spika Wetang’ula awataka wabunge wapitishe sheria ya kuweka NG-CDF katika Katiba kuzuia kesi nyingi – Taifa Leo


Spika Wetang’ula awataka wabunge wapitishe sheria ya kuweka NG-CDF katika Katiba kuzuia kesi nyingi

NA CHARLES WASONGA

SPIKA wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula amewahimiza wabunge waharakishe utayarishaji wa sheria itakayoiweka Hazina ya Ustawi ya Maeneo Bunge (NG-CDF) katika Katiba kuikinga na kesi nyingi za kuipinga.

Alisema tangu kuanzishwa kwa hazina hiyo mnamo 2003, imesaidia pakubwa katika ufadhili wa miradi mingi ya maendeleo katika maeneo bunge.

Hazina hiyo ilianzishwa baada ya kupitishwa kwa Sheria ya CDF, inayoitaka serikali kutenga angalau asilimia 2.5 ya mapato yake kwa hazina hiyo.

“Kwa hivyo, nawahimiza wabunge kwa kauli moja kupitisha sheria itakayoiweka hazina katika Katiba ili kuhakikisha pesa za maendeleo zinapatikana kwa wakati,” Bw Wetang’ula akasema.

Spika huyo amesema hayo mjini Mombasa mnamo Jumatano, Februari 1, 2023 alipokuwa akiwahutubia wabunge wakati wa semina ya kuwahamasisha wabunge jinsi ya kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Semina hiyo imedhaminiwa Bunge la Kitaifa pamoja Muungano wa Mabunge ya Mataifa wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA).

Wito wa Spika Wetang’ula amejiri siku chache baada ya wabunge kususia mkutano wa mafunzo kushinikiza hazina ya kitaifa itoe fedha za CDF.

Ni baada ya mgomo huo, wa wiki jana, ambapo Hazina ya Kitaifa ilitoa Sh4 bilioni za hazina hiyo.

Wabunge walilalamika kwamba wanafunzi ambao hutegemea pesa hizo kulipiwa karo walikuwa wakihangaika.

“Hatuwezi kuendelea na mkutano hapa Mombasa huku kustarehe kwa pesa za umma ilhali watoto ambao wanategemea basari ya CDF hawajaripoti shule kwa kukosa karo. Hili suala la CDF sio la kisiasa bali linahusisha masilahi ya watoto kutoka jamii masikini katika maeneo bunge yetu,” akasema Mbunge wa Seme James Nyikal.

Mwishoni mwa mwaka jana, Mbunge wa Matungulu Stephen Mule (Wiper) na mwenzake wa Gichugu Gichimu Githinji (UDA) walianzisha mchakato wa kuandaa mswada wa marekebisho ya Katiba ili  kuweka NG-CDF katika Katiba.

Hiyo ni kufuatia uamuzi wa Mahakama ya Kuu sheria ya CDF, 2003 inakiuka Katiba na hivyo ni haramu.

Ni kwa msingi wa uamuzi huo ambapo Hazina ya Kitaifa ilidinda kutoa fedha za hazina ya NG-CDF kuanzia tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa kifedha wa 2022/2023.

Lakini mnamo Desemba 2022, Mwanasheria Mkuu Justin Muturi alishauri kuwa Hazina ya Kitaifa inaweza kuendelea kutoa fedha za hazina hiyo chini ya Sheria ya NG-CDF, 2015 ambayo haikuwa imeharamishwa.



Source link

Comments

comments

Facebook

Trending