Connect with us

General News

Tazama jinsi babake Diamond alivyobadilika baada ya kurekebisha uhusiano na mwanawe ▷ Kenya News

Published

on


Nyota wa Bongo Diamond Platinumz na babake Mzee Abdul washerehekea na kujivinjari majuma machache baada ya wawili hao kuunda uhusiano wao baada ya uadui wa muda mrefu.

Awali, TUKO.co.ke ilitangaza kwamba wawili hao walikuwa hawaonani wala kuzungumziana kwa zaidi ya miaka 20, jambo ambalo lilimsababishia babake msanii huyo kuishi kwa uchochole licha ya mwanawe kuwa na mali nyingi.

Habari Nyingine: Willy Paul, Nandy wanusurika kifo baada ya gari lao kupinduka nchini Tanzania

Hata hivyo, wawili hao walirekebisha uhusiano wao katika mahojiano ya moja kwa moja katika kituo cha redio cha Wasafi FM, na matunda ya patanisho hilo yamenza kudhihirika wazi.

Picha hizo ambazo zinadhihirisha mwamko mpya kwake Mzee Abdul, ziliwafurahisha wananchi wengi kutoka Tanzania ambao walifichua kwamba amebadilika na kupendeza ajabu.

Habari Nyingine: Makachero wamtia nguvuni mwalimu mkuu aliyeongoza shambulizi dhidi ya wanahabari

Baadhi ya wafuasi wake Diamond walimpongeza kwa kusameheana na babake na kuyabadilisha maisha yake.

Wengine wao aidha walifurahia mwamko mpya wa Mzee Abdul na jinsi alivyoonekana mchangamfu.

Kulingana na picha hizo zilizoonesha jinsi Mzee Abdul alivyokuwa amechangamka, ni bayana kwamba alihitaji mabadiliko hayo kabla ya hata kupata matibabu.

Wawili hao walirekebisha uhusiano wao uliozongwa na chuki iliyokuwepo baina yao kwa miaka na mikaka baada ya babake msanii huyo kuomba msamaha.

Kwa muda mrefu, Diamond alishambuliwa mitandaoni kwa kumtenga babake ingawaje alipinga madai hayo na kusema uhusiano wao ulikuwa shwari ila babake alijitenga mwenyewe kwa sababu zake za kibinafsi.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending