Connect with us

General News

Utafiti: Miraa ni sumu kwa akili ya binadamu ▷ Kenya News

Published

on


Utafunaji wa miraa unaweza kusababisha matatizo ya kiakili, utafiti umeonyesha.

Kulingana na utafiti uliofanywa na taasisi ya Kemri, miraa ina uwezo wa kumfanya mtu kuwa na matatizo ya kiakili kama vile kushikwa na mazingaombwe.

Utafiti huo ulihusisha wakaazi 831 wa maeneo ya Embu na Meru ambapo walionekana kuwa na matatizo hayo ya kiakili kutokana na matumizi ya miraa kwa muda mrefu.

Habari Nyingine: Penzi hatari: Mkewe Chris Attoh alikuwa ameolewa na wanaume wawili

Utafiti wa Kemri unasema utumiaji wa miraa una madhara ya kiakili. Picha: UGC
Source: UGC

Watafiti walisema watu hao hawakuonyesha matokeo sawa na hayo walipofanyiwa uchunguzi wa matumizi ya pombe ama tumbaku.

Miraa hujulikana na kusisimua mwili kutokana na madini ya alkaloid cathinone.

Habari Nyingine: Somalia: Serikali yafutilia mbali mtihani wa kitaifa baada ya madai kuwa ulisambazwa mitandaoni

Shirika la Afya Duniani mnamo mwaka wa 1980 liliorodhesha miraa kama aina ya mihadarati iliyo na madhara ya kiakili.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke; obed.simiyu@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending