Connect with us

General News

Utata kuhusu mahindi ya GMO wazua maswali tele – Taifa Leo

Published

on


Utata kuhusu mahindi ya GMO wazua maswali tele

– Kwa nini Bw Kuria aliingilia suala la uagizaji wa mahindi ya GMO ilhali jukumu hilo ni la Wizara ya Kilimo?

Kulingana na amri iliyotolewa na Rais Ruto mwezi uliopita, Wizara ya Kilimo ndiyo imepewa majukumu la kutengeneza sera kuhusu chakula nchini, kusimamia hifadhi ya chakula na vyakula vya GMO na mazao.

– Je, Bw Kuria anazungumza kwa niaba ya nani?

– Kwa nini Waziri wa Biashara alitangaza kuleta mahindi ya GMO bila kushauriana na mwenzake wa Kilimo Mithika Linturi?

– Mbona Waziri wa Kilimo Mithika Linturi amesalia kimya kuhusu suala la GMO ilhali chakula kiko chini ya wizara yake?

– Ni nani analenga kunufaika kibiashara na mahindi ya GMO?

– Bw Kuria alijuaje kwamba magunia milioni 10 ya mahindi ndiyo yanahitajika kumaliza njaa nchini?

– Mbona mahindi yasinunuliwe kutoka kwa wakulima wa humu nchini na kuyapeleka kwa Wakenya wanaohangaishwa na njaa?

– Kwa nini wabunge kutoka maeneo yanayokuza mahindi – Bonde la Ufa na Magharibi – wanapinga mahindi ya GMO mbele ya vyombo vya habari ilhali wanaweza kumwendea Rais Ruto moja kwa moja na kumueleza kilio chao?

– Mbona Bw Kuria hajachapisha taarifa ya kuruhusu wafanyabiashara kuleta mahindi ya GMO licha ya kuahidi kuwa angefanya hivyo Ijumaa iliyopita?

– Wapi orodha ya wafanyabiashara ambao wamepewa kibali cha kuleta mahindi ya GMO nchini?