Connect with us

General News

Utovu wa usalama watishia KCPE, KCSE – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Utovu wa usalama watishia KCPE, KCSE – Taifa Leo

Utovu wa usalama watishia KCPE, KCSE

FLORENCE KOECH NA JACOB WALTER

WALIMU wasiokuwa wenyeji sasa wanatoroka eneo linalokabiliwa na utovu wa usalama kwenye Bonde la Kerio wakati ambapo mashirika ya kitaifa yameitaka serikali iahirishe mitihani ya kitaifa inayoanza wikKCSEi ijayo.

Vyama vya walimu na makundi ya kutetea haki za kibinadamu yanaitaka serikali iahirishe mitihani ya KCPE na KCSE katika eneo hilo hadi usalama uimarishwe na hali kurejea kawaida.

Wanasisitiza hiyo ndiyo njia pekee ya kuhakikisha kuwa watahiniwa wote wanafanya mitihani yao katika

mazingira tulivu. Ripoti zinaarifu kuwa zaidi ya walimu 30 ambao si wenyeji, wametoroka kutoka shule za eneo hilo hali ambayo imelemeza kabisa shughuli za masomo.

Walimu waliohepa wakiwemo walimu wakuu wanasema walifanya hivyo baada ya kukosa kuhakikishiwa usalama wao kutokana na mashambulizi ambayo yamekuwa yakiendelea mara kwa mara.

Uvamizi wa majangili na wezi wa mifugo umesababisha vifo vya zaidi ya watu 30 tangu mwanzo wa mwaka huu huku mamia wengine wakilazimika kuhama makwao ili kujinusuru.

Shughuli za masomo katika zaidi ya shule 20 za msingi na upili kwenye maeneobunge ya Baringo Kaskazini

na Baringo Kusini zimelemazwa huku baadhi ya shule hizo zikiwa hazikufunguliwa kwa muhula wa tatu unaokamilika leo.

Matukio ya uvamizi wa majangili na wizi wa mifugo kati ya jamii za Elgeyo-Marakwet na Pokot, nayo yamesababisha wenyeji kuhama makwao wakihofia mashambulizi ya kulipiza kisasi.

Utovu wa usalama ulitokota zaidi mnamo Jumamosi iliyopita baada ya zaidi ya watu wanane kuuawa kwenye visa vya ufyatulianaji wa risasi kati ya Wapokot na Wamarakwet kwenye Bonde la Kerio. Watu kadhaa walibaki na majeraha ya risasi kutokana na tukio hilo.

Nao wanafunzi 13 na walimu wawili kutoka Shule ya Sekondari ya Tot inayopatikana Bonde la Kerio walijeruhiwa kwenye kisa cha mwezi uliopita ambapo dereva wa basi lao alipigwa

risasi na kufa. Uvamizi huo ulitokea Chesuman kwenye barabara ya Biretwo-Tot.

Katika eneo la Turkana Mashariki, Shule ya Msingi ya Napeitom ilifungwa kufuatia kisa cha uvamizi wa majangili huku mwalimu mmoja akiwa kati ya walimu wanne waliouawa kwenye uvamizi uliotokea wiki hii.

Kutokana na hali tete ya kiusalama, maafisa wa Chama cha Walimu Nchi – ni (Knut) na kile cha KUPPET walitangaza kuwa walimu wanaohudumu Kaskazini mwa Bonde la Ufa watasusia kusimamia mitihani iwapo hawatahakikishiwa usalama wao.

Maafisa hao hasa walitaja shule za msingi na upili zinazopatikana Bonde la Kerio na zinazopakana na kaunti za Baringo, Pokot Magharibi na Elgeyo-Marakwet kama ambako masomo yalilemazwa kutokana na uvamizi wa majangili unaoendelea hata mchana.