Connect with us

General News

Video ya mcheshi Eric Omondi akiuza jezi za Manchester United yasambazwa ulimwengu mzima ▷ Kenya News

Published

on


Mcheshi maarufu wa humu nchini Eric Omondi amesisimua mitandao ya kijamii baada ya video yake akiuza jezi za klabu ya Manchester United kuenezwa ulimwengu mzima

Kwenye video hiyo Eric alijifanya mchuuzi wa jezi za soka huku wanunuzi kadhaa wakiwa wamesimama kando yake.

Habari Nyingine: Pata ufahamu zaidi kuhusu ukomohedhi

Omondi anaanza kwa kuuza jezi za klabu ya Manchester City, Chelsea na Arsenal kwa bei ghali na wanunuzi wanaonekana wakizinunua kwa haraka ila anapoaanza kuuza zile za Manchester United, wanunuzi wanamtazama wakionekana kuchukizwa.

Habari Nyingine: Kutana na mwanamke ngangari, rubani asiyekuwa na mikono

Anauza jezi hizo kwa bei ya chini ila hakuna anayenunua, anaamua kupatiana jezi hizo bila malipo na kila mnunuzi anahepa, hawataki hata kuguza jezi hizo.

Video hiyo uliwafurahisha mashabiki wengi mitandaoni wakiwemo wale wa nchi ya ng’ambo.

Licha ya kutoa video hiyo inayokejeli klabu ya Manchester, Omondi ni shabiki sugu wa klabu hiyo.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Tazama habari zaidi kutoka TUKO TV

Source: Tuko Newspaper

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending