Connect with us

General News

Wabunge kukutana tena Jumanne kufufua hoja iliyozimwa na Tangatanga – Taifa Leo

Published

on


Wabunge kukutana tena Jumanne kufufua hoja iliyozimwa na Tangatanga

Na CHARLES WASONGA

SPIKA wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi ameitisha kikao cha bunge Jumanne wiki ijayo baada ya kupokea ombi rasmi kutoka kwa Kiongozi wa Wengi Amos Kimunya.

“Afisi yangu imepokea ombi kutoka kwa kiongozi wa wengi leo (jana) alasiri akiniomba niitishe kikao cha bunge ili awasilishe hoja ya kuwataka wabunge wabatilishe uamuzi wa Jumanne. Nimekubali ombi hilo na kuitisha kikao Jumanne Februari 1, 2022 kuanzia saa nane alasiri,” akasema kwenye taarifa.

Bw Muturi aliahirisha kikao cha bunge hilo Jumanne baada ya wabunge wandani wa Naibu Rais William Ruto kuangusha hoja ya uteuzi wa wanachama wa Kamati ya Kuratibu Shughuli za Bunge (HBC).

Hii ni kwa sababu bunge halikuwa na ajenda yoyote ya kushughulikia kwa sababu kamati hiyo ndiyo huratibu miswada, hoja na masuala mengine ya kujadiliwa.

“Sina jingine ila kuahirisha kikao cha bunge baada ya kuangushwa kwa hoja hii. Hoja sawa na hii inaweza tu kurejeshwa bungeni baada ya miezi sita,” Bw Muturi.

Hiyo itakuwa ni mwishoni mwa Juni 2022, wiki tano kabla ya tarehe ya uchaguzi, Agosti 9.

“Hata hivyo, Kiongozi wa Wengi Amos Kimunya anaweza kuwasilisha ombi afisini mwangu kuomba bunge lifanye kikao kubatilisha uamuzi wa leo (Jumanne),” Bw Muturi akasema.

Wabunge waliopendekezwa kuhudumu katika kamati hiyo ni; Joyce Emanikor (Mbunge Mwakilishi wa Turkana), Kawira Mwangaza (Mbunge Mwakilishi, Meru), Shadrack Mose (Kitutu Masaba), Abdikarim Mohamed Osman (Fafi), Dkt Makali Mulu (Kitui Mashariki), Mishi Mboko (Likoni) na Mbunge Maalum Godffrey Osotsi.

Mivutano ya kisiasa

Jumatano, Spika Muturi alikiri kwamba hoja hiyo ya kuundwa upya kwa kamati HBC iliangushwa kutokana na mivutano ya kisiasa kati ya wandani wa Dkt Ruto na kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi kwa upande mmoja na wandani wa Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga kwa upande mwingine.

“Nilipokuwa nikiondoka ukumbini niliwasilisha wabunge waliopinga majina ya wanachama wapya ya kamati ya HBC, wakiimbia ‘earthquake…. Earthquake’ ishara kwamba hatua hiyo ilichochewa na hali ya kisiasa,” akawaambia wanahabari jana katika mkahawa wa Serena, Nairobi.

Mvutano huo unatisha kukatatiza mchakato wa utayarishaji bajeti ya mwaka wa kifedha wa 2022-2023 kufadhili shughuli muhimu za serikali kama vile ulipaji wa mishahara wa watumisha wa umma, polis na wanajeshi.

Vile vile, ufadhili wa uchaguzi mkuu ulioratibiwa kufanyika Agosti 9, 2022 unaweza kutatizwa kwa sababu Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) itategemea mgao wa fedha zilizopitishwa na wabunge.Source link

Comments

comments

Facebook

Trending