Connect with us

General News

Wafanyabiashara wa miraa bado wanapunjwa na magenge ambayo Dkt Ruto aliahidi kuangamiza – Taifa Leo

Published

on


TUSIJE TUKASAHAU: Wafanyabiashara wa miraa bado wanapunjwa na magenge ambayo Dkt Ruto aliahidi kuangamiza

MNAMO Septemba 12, 2022 Rais William Ruto – siku moja kabla ya kuapishwa – aliahidi kupambana na magenge ya matapeli ambayo hunyanyasa wafanyabiasha wa miraa nchini, haswa wanaouza zao hilo nchini Somalia.

Aliahidi kufanya hivyo ndani ya mwezi mmoja baada ya kuingia Ikulu.

Akiongea katika ibada ya shukrani katika eneo bunge la Igembe Kusini, Kaunti ya Meru, Dkt Ruto alisema serikali yake itahakikisha wakulima na wafanyabiashara wa miraa wanafaidi.

Lakini zaidi ya miezi mitatu baada ya Rais kuanza kuhudumu, wafanyabiashara wa zao hili bado wanapunjwa na magenge hao hao ambao Dkt Ruto aliahidi kuangamiza “ndani ya mwezi mmoja”.

Wauzaji wa miraa katika mataifa ya ng’ambo bado wanalalamika kwamba wanatozwa ada ya Sh550 ya faida wanayopata kwa kila mfuko wa kilo 50 ya miraa wanayouza nchini Somalia.

Pesa hizo zinatozwa na madalali jijini Nairobi na Mogadishu.

Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Miraa wa Nyambene (Nyamita), Bw Kimathi Munjuri, sasa anamtaka Rais Ruto, kupitia wizara za Kilimo na Biashara, kukumbuka kukomesha uovu huo ambao unaendelezwa na madalali hao wanyanyasaji.Source link

Comments

comments

Facebook

Trending