Connect with us

General News

Wakenya wachemka baada ya Gavana Nyong’o kuomba Raila msamaha

Published

on


– Raila alizuru eneo la Ombei na kuzomewa na wakazi

– Gavana Nyong’o ametumia pesa za umma kuomba msamaha kupitia gazeti hata hivyo hatua hiyo imewakera baadhi ya Wakenya

Gavana wa Kaunti ya Kisumu Anyang Nyong’o amejipata taabani baada ya kutumia pesa za kaunti kununua nafasi kwenye magazeti mawili ya humu nchini kuomba msamaha kwa kiongozi wa ODM Raila Odinga.

Gavana huyo aliomba msamaha baada ya wakazi wa Muhuroni eneo la Ombeyi kumzomea Raila wakipinga mpango kujenga viwandakabla ya kuwalipa vidia kwa mashamba yao yaliyochukuliwa kwa ajili ya mradi huo.

Habari Nyingine: Raila Odinga ajipata pabaya Muhoroni, wafuasi wamkemea vikali wakimtaja kuwa msaliti

Msamaha wa Gavana Nyong’o ambao ulichapishwa kwa mojawapo ya magazeti humu nchini. Picha: Facebook
Source: Facebook

Raila alikuwa amezuru eneo hilo Jumatatu, Mei 13, akiandamana na Waziri James Macharia wa Uchukuzi wakati ambapo kundi la vijana lilimkemea na kumwita msaliti.

Kwenye msamaha huo uliochapishwa magazetini, Nyong’o alisema tukio hilo lilipangwa na baadhi ya wanasiasa.

Hata hivyo hatua ya kutumia pesa za umma kwa njia hiyo imeonekana kuwakera baadhi ya Wakenya.

Hapa ni sehemu ya michango yao kuhusu msamaha wa gavana Nyong’o kwa Raila.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke; obed.simiyu@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram:

Source: Tuko.co.ke





Source link

Comments

comments

Facebook

Trending