Connect with us

General News

Waluke: Raila ni kiongozi mwenye mikosi ▷ Kenya News

Published

on


– Raila alifanya Kenya kunyimwa mkopo

-Ni kiongozi mwenye mikosi

-Amekuwa akiitisha mageuzi ya kikatiba kujinufaisha

Mbuge wa Siria John Waluke amesema kiongozi wa ODM Raila Odinga alifanya Rais Uhuru Kenyatta kupoteza mkopo kutoka kwa Uchina.

Mbunge huyo wa Jubilee alisema Raila ni mtu mwenye mikosi na ndiyo sababu ilifanya serikali ipoteze nafasi ya mkono wa kuendeleza reli ya kisasa kutoka Naivasha hadi Kisumu.

Mbunge John Waluke ambaye amemkashifu Raila akisema anataka kujinufaisha na mageuzi ya kikatiba. Picha: UGC
Source: Facebook

Kulingana na video moja na gazeti la Nation iliyowekwa mtandaoni Jumapili, Mei 12, Waluke alisema Rais Uhuru Kenyatta angepokea mkopo huo iwapo hangeandamana na Raila Uchina kwenye safari ya kuomba fedha hizo.

Habari Nyingine: Rubani atumia ujuzi kuokoa abiria 89 baada ya ndege kupata hitilafu

“Raila ni mtu mwenye mikosi na ndiyo sababu Kenya haikupata mkopo kutoka kwa Uchina hivi majuuzi alipoandamana na rais Kenya nchini humo. Kama Uhuru angekuwa peke yake, angepewa fedha hizo,” mbunge huyo alisema.

Kulingana na mbunge huyo, serikali ya Uchina ilikataa kutoa mkopo huo kwani wafuasi wa Raila walikuwa wamebomoa reli humu nchini wakati mmoja.

“Serikali ya Uchina inamjua Raila kama anayeongoza uharibifu wa mali. Uchina ilimwangalia na kuamua haiwezi kutoa mkopo,” aliongeza.

Mwanasiasa huyo ambaye ni mfuasi wa naibu wa rais William Ruto alimkosoa Raila kwa kile alisema ni kuitisha mageuzi ya kikatiba ili kujinufaisha kisiasa.

Habari Nyingine: Tanasha atoboa siri ya vile Diamond alimtia ‘boxi’

“Raila ndio aliongoza mageuzi yaliyoleta katiba ya sasa, na hata kabla ya kuitekeleza ameanza tena kuitisha mageuzi,” Waluke alisema.

Waluke alikuwa mfuasi wa Raila kwenye chaguzi za 2007 na 2013 kabla ya kutofautiana mwaka wa 2017 na akajiunga na Jubilee.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke; obed.simiyu@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko.co.ke

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending