Wanaume wengi kupitia mitandao ya kijamii wamelalamika kwamba ni vigumu kuelewa tabia ya wanawake wengine
Kulingana na utafiti uliofanywa hapa TUKO.co.ke, wanaume wengi hushangazwa na wanawake kwani kwa wakati mmoja wanaweza kuwa na furaha, wakati mwingine wamekasirishwa na jambo ambalo sio hata la maana.
Baadhi ya wanaume walishangazwa ni vipi wanawake wengi hulia wanapokasirishwa na jambo ndogo ambalo halina msingi.
Wanaume wataja mambo ambayo yamefanya washindwe kuelewa wanawake
Source: Facebook
Mtumiaji mmoja wa mitandao ya kijamii aliyetambulika kama Binghi Mwende alisema yeye hushangazwa sana ni vipi wanawake huweka mikebe ya Yohgurt yenye washatumia kwenye mikoba yao badala ya kuitupa.
Mwingine aliyetambulika kama Mbugua Moses alitaka kujua iwapo mwanamke huisi uchungu akijifungua au wengine hujifanya tu.
Wanaume wataja mambo ambayo yamefanya washindwe kuelewa wanawake
Source: Facebook
Swali lililoshangaza wengi ni mbona wanawake hupatwa na hali ya dharura kila mara mpenzi anapomtumia nauli ya kwenda kumtembelea.
Read ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa inayoweza kubadilisha maisha ya mtu na ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690 na Telegram: Tuko news.
Tazama habari habari zaidi kutoka TUKO TV
Subscribe to watch new videos
Source: Kiswahili.tuko.co.ke
Source link