Connect with us

General News

Waziri Amina Mohammed amuandalia rafikiye sherehe ya kufana ya ‘Baby Shower’ ▷ Kenya News

Published

on


Waziri wa Michezo Amina Mohammed alimuandalia rafiki wake wa karibu sherehe nono ya ‘Baby Shower’ ambayo ilihudhuriwa na watu mashuhuri pekee

Sherehe hiyo ambayo ilifanyika Jumamosi Julai 13, pia ilihudhuriwa na marafiki wa karibu wa balozi Yvonne Khamati.

Habari Nyingine: Katibu mkuu wa Jubilee Raphael Tuju apuuza madai ya Ruto, kuendelea kumshauri Raila

Akiwa mwenye furaha, Yvonne alichapisha picha kadhaa kwenye mtandao wa Instagram akimshukuru Waziri Amina kwa kuandaa sherehe hiyo.

”Cheiii… dadangu mkubwa waziri Amina Mohammed akiamua kuniandalia sherehe nono na nisiyotarajia ya Baby Shower,” Alisema Khamati.

Habari Nyingine: Moses Kuria amjibu Ruto kuhusu Tuju kuwa msaliti ndani ya Jubilee

Wengine waliohudhuria sherehe hiyo ni Waziri Amina mwenyewe, mumewe Yvonne na binti wao.

Kulingana na picha tulizoziona hapa TUKO.co.k, ni wazi kuwa Amina aligharimika vilivyo ili kufanikisha sherehe hiyo.

Habari Nyingine: Linus Kaikai: Serikali ya Uhuru ni ya ‘kitoto’ na ‘ujinga’

Haya yanajiri miezi michache tu baada ya Yvonne ambaye ni balozi wa Kenya nchini Somalia kuposwa na mpenziwe Jumamosi, Mei 5, 2019.

Read: ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending