Connect with us

General News

Wema Sepetu adai Ali Kiba ni mwanamuziki bora kumliko mpenzi wake wa zamani Diamond Platinumz ▷ Kenya News

Published

on


Mwanamitindo na mwigizaji maarufu Wema Sepetu ametoa kauli yake kuhusu ni nani gwinji wa muziki kati ya aliyekuwa mpenzi wake Diamond Platinumz na msanii Ali Kiba

Kulingana na Sepetu, Ali Kiba anaelewa vema muziki kumliko mpinzani wake mkuu Diamond Platinumz.

Akizungumza kwenye mahojiano na Global Publishers, Wema alisema haoni hoja kubwa ya yeye kujadili nani kati ya wanamuziki hawa ni bora kwani hakuna anayeweza kumshinda Kiba.

Aidha , Wema alidai kuwa hana wasiwasi kumtaja kiba kuwa mwanamuziki Bora kwani tayari ashamtaarifu Diamond kuhusiana na swala hili na analifahamu vema.

” Watu wengi huwa hawaelewi, siwezi nikaficha hisia zangu, mimi napenda sana nyimbo za Kiba na Diamond mwenyewe anafahamu jambo hili, kila mtu yuko na uhuru wa kupenda mwanamuziki yeyote, mimi huhisi vizuri nikisikiliza muziki wa Kiba,” Sepetu alisema

Madai ya Wema yanatokea huku ikieleweka wazi kuwa wanamumziki hao wawili ni mahasidi wakuu.

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending