Connect with us

General News

Wito waziri Machogu aruhusu wanafunzi kupata muda mwingi wa elimu darasani – Taifa Leo

Published

on

Wito waziri Machogu aruhusu wanafunzi kupata muda mwingi wa elimu darasani – Taifa Leo


Wito waziri Machogu aruhusu wanafunzi kupata muda mwingi wa elimu darasani

NA LAWRENCE ONGARO

WASHIKADAU wa shule za msingi za kibinafsi katika eneo la Thika Magharibi walikongamana kujadili kuhusu hali ya elimu kwa ujumla.

Wakurugenzi wapatao 60 wa shule za kibinafsi chini ya mwavuli wa Kenya Private Schools Association, walijadili maswala mengi kuhusu wanafunzi, walimu na usimamizi wa masomo kwa ujumla.

Hivi majuzi Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu alitoa mwelekeo wa saa za wanafunzi kuhudhuria madarasa kutoka asubuhi hadi jioni.

Wanafunzi watakuwa wakiripoti darasani saa mbili za asubuhi na kuondoka darasani saa kumi kasorobo jioni.

Mwenyekiti wa muungano wa walimu wa Kenya Private Schools Association Thika Magharibi, Bi Mary Kirika, alisema pendekezo hilo linastahili kujadiliwa na washikadau wa elimu ili waweze kuafikia msimamo mmoja.

“Pendekezo hilo la saa za kuhudhuria vikao vya masomo darasani lina changamoto tele kwa sababu shule za kibinafsi zina mipango yao ya usafiri kwa wanafunzi wao,” alisema Bi Kirika.

Alisema masaa hayo hayatalingana na  muda huo uliopendejezwa na waziri .

“Iwapo tutafuata agizo la waziri kutakuwa na changamoto kutokana na usafiri. Kila shule ya kibinafsi imeweka mpangilio wake wa usafiri na hiyo italeta utata kiasi,” alisema Bi Kirika.

Alisema usalama wa wanafunzi pia unastahili kuchungwa wakati wowote wanapokwenda shuleni.

“Suala la wanafunzi kufika shuleni wakati ufaao ni jukumu la shule, madereva, wazazi na hata walimu. Kwa hivyo suala hilo linastahili kujadiliwa kwa kina na washikadau wote,” akasema.

Alisema changamoto kubwa wanayopitia kama washikadau ni ukosefu wa walimu wenye vyeti vya kutoka TSC.

Hata hivyo alisema mfumo wa masomo ya msingi kuelekea Gredi ya Saba una changamoto tele hasa kwa walimu huku akitaka hamasisho zaidi.



Source link

Comments

comments

Facebook

Trending