Connect with us

General News

Ben Githae aeleza vile alitoka nje ya ndoa yake

Published

on


Ben Githae ni mwana mziki wa nyimbo za injili ambaye amejulikana sana katika sekta ya usanii. Aliweza kukumbwa na jambo la kuwa alikuwa ametoka nje ya ndoa na kupata watoto mapacha wawili na mpango wake wa kando.

Aliweza kusema kuwa amekua katika ndoa yake na mke wake kwa muda wa miaka 18.

Ilikuaje: Cashy aeleza kilichomfanya atengane na mume wake Khaligraph

“Nimekaa kwa ndoa kwa miaka 18, tuliweza kupata watoto wawili, baada ya Rose Wanjiru kuweka mambo wazi kuwa niliweza kupata mapacha wawili na yeye kuliweza kuwa na mvutano kati yangu na mke wangu,

“Tuliweza kutatua mambo mengine nikiwa na mke wangu na mengine tukaamua kukaa nayo,” Alieleza Ben.

Ben aliweza kukataa madai kuwa aliweza mshawishi Rose aweze kuavya mimba ili watu wasiweze kujua.

Alisema kuwa mama wa watoto wake ambaye ni mpango wake wa kando aliweza kumtishia maisha ndiposa aweze kumfanyia mambo ama afichue siri kwa vyombo vya habari.

“Rose aliweza nitishia maisha ili nimfanyie mambo kadhaa na nisipomfanyia alikuwa ananiambia ataweza kuambia vyombo vya habari kuwa ako na mtoto na mimi,” Ben alizungumza.

Ben alisema kuwa katika familia yake hakukuwa na mvutano, jambo ambalo linge msababisha aweze kuenda nje bali ni msukumo tu uliweza kumsukuma kuenda nje ya ndoa.

Ilikuaje: Nilizaliwa na kaka na dada, Musa Ingosi asimulia

“Wacha niseme ni msukumo tu uliniwezesha niende nje ya ndoa, na wala sikua nimekosana na mke wangu ama hakukuwa na mvutano wowote ilikuwa tu tabia mbaya,” Alisema Githae.

Mwanamke huyo wa mpango wa kando aliweza kusema kuwa mwanamziki huyo hakuweza kumsaidia baada ya kujifungua mapacha hao.

Jambo ambalo Githae amelikanusha na kusema kuwa ameweza kuwasaidia watoto wake hadi sasa hivi ambapo wana miaka mitatu.

Ilikuaje: Joyce asimulia vile aliolewa akiwa na miaka 11

“Mimi sikukataa kuwasaidia watoto wangu na kama sheria invyosema nina ruhusa ya kuwaona, huwa nawapigia simu ninaongea na wao,

“Jambo hilo lilipotokea uhusiano wangu na mke wangu uliweza kutingika kwa muda sasa, niliweza kurekibishwa na wazazi kwa maana wananiona mimi bado ni mtoto wa kukosolewa,

“Niliweza kusushwa moyo kwa ajili ya jambo hilo lakini watoto wangu walinipa nguvu,” Alisimulia Ben.

Mwanamziki huyo alisema kuwa nyimbo zake nyingi zimeweza kutumika dhidi yake kwa mateto mengi ambayo yaliweza kuwekwa wazi.

Alisema pia alipatana na mke wake wa mpango wa kando katika sherehe na wala hakuweza kumchumbia bali alijipata pamoja na kisha kumpa uja uzito.

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending