Connect with us

General News

Bibi aliniacha baada ya kupoteza kazi yangu

Published

on


Brian aliomba apatanishwe na mkewe Gladys, ambaye alitoweka pindi tu alipopoteza kazi yake.

“Bibi alienda mwezi wa pili mwaka huu na sijui kama amepata mume mwingine. Tumekuwa tukizungumza na mamake lakini yeye huniambia kuwa hana nambari yake lakini najua hadai kunipea number.” Alieleza Brian.

Tulikuwa na yeye Nairbi na kazi ikaisha, sasa mzee wangu akaniambia kama kazi imepunguka nienda nyumbani anipe kazi, nami nikamweleza mke wangu abaki Nairobi ili nikatafute kibarua.

Nilipopata kazi nikamuita mahali nilipo na baada ya siku tatu siku mbili akatoweka tena. Sasa sijui mbona.” Aliongeza.

Wawili hao wamekuwa kwa uhusiano wa miaka miwili lakini bado hajalipa mahari ingawa alikuwa kwenye shughuli ya kulipa mahari.

Wamejaliwa mtoto mmoja.

Alipopigiwa simu, mamake alijibu simu na kusema kuwa Gladys tayari ameolewa tangia wawili hao watengane.

Isitoshe, alifichua kuwa Brian alikuwa akimpiga kila wakati na hadi kuna siku alimfukuza na wakapelekana kwa polisi.

“Brian alikuwa amepewa number lakini alianza matusi na hapo akawekwa kwa blacklist.” Alieleza Mama Gladys.

 

Source link

Comments

comments

Advertisement
Loading...
Loading...

Facebook

Loading...

Trending

Kenyan Digest