PATANISHO: Bibi yangu alitoroka sababu sinunui chakula cha kutosha
Ngugi alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe, bi Wanja, ambaye walikosana baada yake kusema kuwa bwanake hamshibishi.
“Alikuwa anasema eti simnunulii chakula na hashibi, ya pili eti silipii mtoto karo na hayo mengine siwezi jua zaidi ya hapo. Sasa ningependa kujua na nimuombee msamaha.” Alieleza bwana Ngugi.
Jamaa alijitetea akidai hiyo siku aliondoka, alibeba shopping yote aliyokuwa amefanya.
Isitoshe imagine mimi ni dereva na naenda na gari miezi minne bila kulipia bima ili ile pesa napata kidogo mke wangu na watoto wale, imagine kama nafanya hayo yote ningependa kujua nilifanya nini ili atoroke ili niombe msamaha. Aliongeza.
Wawili hao wamejaliwa watoto wawili baada ya mtoto mmoja kuaga dunia. Mkewe aliondoka na watoto na kwenda Kayole.
Tangia mkewe aondoke Jumapili iliyopita amejaribu kuzungumza na mkewe na baada ya kumpigia simu mkewe alijibu ‘Nikusaidie aje’ na hakufurahishwa na hilo jibu.
Hata hivyo, Wanja alikataa kuzungumza nasi aliposkia ni kitengo cha Patanisho.
Pata uhondo kamili.



