Waliweza kupatana na mume wake Khaligraph Jones akiwa katika sekta ya usanii kisha akaweza kumchumbia na kumuoa kwa miaka mitano.
Baada ya miaka mitano Cashy aliweza kupitia vurugu katika familia yake na kupigwa au kuchapwa na mume wake baada ya kuvumilia kisha kuamua kuwa ametosha kuchapwa.
“Nilivumilia sana na sikuwa naambia mtu yeyote kwa sababu nilikuwa najali Khaligraph na pia, yaani vile watu watamchukua na vile watamuona katika sekta ya usanii,
“Nilitoka katika ndoa hiyo kwa sababu kuna mambo ambayo hayakunipendeza licha ya kuchapwa na Khaligraph,”Alisimulia Cashy.
Cashy
Alisema kuwa akiwa katika uhusiano huo aliona hawezi kukua kimawazo pia katika usanii wake na pia aliweza kuadhirika kwa njia nyingi.
“Niliona nikizidi kukaa katika uhusiano huo na kisha kunyamaza unyama ambao nilikuwa nafanyiwa, nilieza kuadhirika kimawazo,
“Na pia nilikuwa na majeraha katika mwili wangu,”Alizungumza Cashy.
Kitumbua kiliingia mchanga wakati aliweza kufungiwa kwa nyumba na mwanamziki huyo kisha akachukua simu zake ili asiweze kutoka nje na watu kumuona yaliyomtendekea.
Aliweza kusema kuwa Khaligraph wakati huo hakuwa anatumia dawa zozote za kulevya ndio aweze kumpiga Cashy kichapo cha mbwa.
“Niliweza kufungiwa kwa nyumba na kisha simu zangu kuchukuliwa ili nisiweze kutoka nje ndio watu waniulize kilicho nitendekea,
“Niliamua kuongea na kutoka kwa maana nilikuwa naumia, na nikaona siwezi vumilia vita tena,” Cashy alisema.
Alipojitokeza na kuweka wazi mambo ambayo alikuwa anapitia wasanii wengi na watu wengi waliweza kumtumia jumbe za pole katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram.
“Wasanii wengi waliponihimiza na kunitia moyo niliona kuna watu wengi wanapitia mambo magumu kuliko ambacho nilipitia,”Aliongeza Cashy.
Aliweza kuwahimiza wanawake ambao wanapitia jambo kama lake wasiweze kunyamaza bali waweze kuzungumza na mtu.
Aliweza kusema kuwa alikuwa anaogopa kuwaambia wazazi wake kwa maana yeye ndiye kifungua mimba katika familia yao na hakuna vile angeweza kumwambia baba yake alichokuwa anapitia.
Baada ya kuzungumza na wazazi wake kwa sasa anaweza kusimulia kilicho mpata kwa dada zake. Cashy aliweza kuendelea na maisha kisha kupata mtoto mmoja.
Alisema kuwa hivi karibuni ataweza kuolewa na kuacha yaliyopita nyuma.