Connect with us

General News

Eddy Kimani asimulia vile alivyo jipata nje ya ndoa

Published

on


Eddy Kimani alikuwa mtangazaji aliyekuwa amejulikana kwa sana na mashabiki pia wananchi. Mnamo siku moja aliweza kufichua kuwa aliweza kuenda nje ya ndoa hii ni baada ya kupitia changamoto za maisha.

Mnamo mwaka wa 2014-2017, Eddy aliweza kupata kazi eneo la Nakuru huku akiacha familia yake Nairobi.

Ilikuaje: Ben Githae aeleza vile alitoka nje ya ndoa yake

“Niliweza kupata kazi Nakuru ya mwelekezi wa mazungumzo wa kaunti ya Nakuru, nikiwa katika kazi hiyo niliweza jiingiza kwa mambo ambayo hayakunielewa,

“Mambo ambayo yalikuwa hayaeleweki, niliweza kuchukua mikopo kutoka kwa benki tofauti ili niweze kujikimu na kujifariji kimaisha,

“Ni mambo ambayo yalichangia ndoa yangu kusambaratika,” Alisimulia Eddy.

Ilifika wakati kazi hiyo iliweza kuisha niliweza kufukuzwa katika nyumba yangu kwa kukosa kulipa kodi, pia aliweza kuchukua mikopo ili aweze kukuza biashara zake.

 

“Nilichukua mikopo ili nikuze biashara zangu lakini ilifanya kugeuka na sikuweza kurudisha pesa hizo kwa hivyo mshahara wangu ulikuwa unachukuliwa wote kwa ajili ya madeni,

“Niliweza kupatikana nikiwa nje ya ndoa na mke wangu, ambapo iliwezesha ndoa yangu pia  kusambaratika na kisha kuachana na mke wangu,

“Niliweza kurudi kuishi na mama yangu mzazi nikiwa na miaka 39, hii ni baada ya kutengana na mke wangu na kila kitu kilikuwa kimeharibika,

“Kwa maana sikua na kazi wala pesa na wakati huo huo nilikuwa nimepoteza familia yangu,” Alizungumza Eddy.

Ilikuaje: Cashy aeleza kilichomfanya atengane na mume wake Khaligraph

Baada ya kuishi na mama yake aliweza kuenda mjini Mombasa eneo la Ukunda alipokuwa akifanya kazi ya vibarua eneo hilo.

“Nilikuwa nafanya kazi ya vibarua, siku moja niliweza enda kukaa katika duka la kutengeneza mikate, kwa maana nilifikiria sikua najulikana maeneo hayo,

“Lakini mtu mmoja aliweza nijua, baada ya muda usiokuwa mrefu tuliweza kujuana, kumbe alikuwa mwenye duka hilo,

“Nilimueleza nilichokuwa napitia kwa zaidi ya muda wa masaa manne, na sikua namjua wala mtambua bali nilimfungulia moyo na kumuambia shida zangu,” Eddy alisema.

Mwanaume huyo aliyefahamika kama Peter ndiye aliweza kufanya maisha ya Eddy kubadilika na kumuonyesha njia mbadala ya kuendelea na maisha alisema Eddy.

Alisema kuwa mambo hayo yaliweza kufanya uhusiano wake na watoto wake na mke wake kufifia.

“Uhusiano wangu na familia yangu ulififia sana, na changamoto ambazo nimepitia zimeweza kunifundisha somo kubwa kuwa familia ni kitu muhimu,”Aliongeza Eddy.

Eddy aliweza kuingia katika utangazaji mwaka wa 2000 katika stesheni ya NTV, alipokuwa mtangazaji wa spoti kisha kuenda katika stesheni ya KBC na kuwa mtangazaji pia.

eddykimaniblackshot

Safari yake ya mwisho ya kuwa mtangazaji iliweza kukamilika katika kituo cha Capital kituo ambacho aliweza kufanya kazi kwa muda.

“Niliweza kujisamehe kwanza kwa mambo ambayo nilikuwa nimefanya, na kuweka mambo ya maana katika mstari wa kwanza,

“Ilifika wakati ambapo niliona kitu cha maana katika maisha yangu nikunywa pombe,” Eddy alisema.

Eddy alisema kuwa ataweza kurudi katika vyombo vya habari Ijumaa ya wiki hii.

 

 

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending