Thursday, 10 September 2026
Kenyan Digest

Jacinta Wanjiku aeleza vile alivyoozwa na mama yake

2 min read
Published 5 March 2019

Jacinta Wanjiku ni mwanamke ambaye amekuwa akijua maisha ya kupika chang’aa tangu alipokuwa mtoto mdogo, kwani alianza kupika pombe akiwa na miaka 13.

Nilianza kupika chang’aa nilipomaliza darasa la nane ata wakati mwingine nilikuwa naenda shule nikiwa nimelewa.

Nili lelewa na baba wa kambo ambapo mama yangu alianza kuniambia nina uhusiano wa kimapenzi na baba yangu.

Hii ni baada ya mama kuingia katika ulevi, ilibidi niweze kuandika barua ya kuomba msamaha kwa jambo ambalo sijui kwa maana nilikuwa mtoto.

Mama aliweza kudai hayo yote kwa maana aliona tunapendana sana na baba,” Alieleza Jacinta.

Ilikuaje: Margaret Wajobi asimulia vile aliweza pitia operesheni mara kumi

Baada ya kumaliza darasa la nane hakuweza kupendezwa na alama alizopata ,aliweza kupelekwa kusomea ufundi wa nguo, huku kila wakati akifukuzwa kwa ajili ya karo ya shule.

“Nilikuwa nafukuzwa kila wakati mama yangu aliniambia amechoka kunisomesha, na kisha kuniita kahaba. Nilikaa nyumbani baada ya muda aliniambia kuna shule ya upili naweza jiunga nayo, nilipoenda nilianza tena kufukuziwa karo.

Baada ya muda mama alikuwa na rafiki mwanaume akaniambia kuwa nitaweza kuenda na yeye ili niende nikasomee kwa nyanya wa jamaa yule.” Alisimulia Wanjiku.

Aliweza kupitia hayo yote baada ya kutoka shule na kuacha kusoma, licha ya kuwa na hamu ya kusoma, aliweza kuandamana na mwanaume huyo hadi kwao bali si kwa nyanya wa mwanaume huyo.

Jacinta aliweza kuambiwa na mama yake kuwa mwanaume huyo atampeleka shule,walipofika baada ya siku mbili mwanaume huyo aliweza kumwambia kuwa yeye ni mke wake.

Ilikuaje: Avril asema hakuzaa kupitia oparesheni bali alizaa kawaida

Aliweza kumuuliza kwa kina na kufichua kuwa alimpa mama yake shillingi 35,000 ili Jacinta awe mke wake.

Aliniambia kuwa anajua ya kwamba amepata bibi na kuanzia wakati huo nilieza kuwa bibi yake, kwa zaidi ya mwaka mmoja,

Singeenda mahali kwa maana sikuwa najua kwa nyanya yangu, baada ya kukaa na yeye kwa muda huo wote, niliweza kujua kwa nyanya yangu.

Nikamuelezea kila kitu kisha kunichukua nikaishi na yeye, nilitoka kwa boma ambayo nilikuwa nimeolewa kwa maana mwanaume huyo hakuwa nyumbani wakati huo,” Wanjiku alizungumza.