Thursday, 10 September 2026
Kenyan Digest

Kantai kuaga dunia baada ya kulazwa hospitali kwa siku mbili

2 min read
Published 28 February 2019

Chris Kantai ni rapper aliyejulikana na mashabiki wake, familia, marafiki na ata mashabiki hawakuamini waliposikia kutangazwa kwa kifo chake.

Kantai alifariki Jumatano majira ya asubuhi baada ya kulazwa hospitalini kwa siku mbili tu. Aliweza kufariki baada ya kupambana na ugonjwa wa shida za mawazo kwa muda mrefu.

RIP: Mtangazaji Mutahaba kufariki akipokea matibabu Afrika Kusini

Chris Kantai

Msanii huyo aliweza pumua pumzi yake ya mwisho akiwa katika hospitali ya St. Francis katika maeneo ya Kasarani, mwakilishi wa familia alisema kuwa Kantai alifariki kwa ajili ya matatiza ya kupumua.

Mmoja wa familia aliye karibu na vyombo vya habari aliweza kusema kuwa Kantai amekuwa na matatizo ya ugonjwa kwa muda mrefu.

“Amekuwa mgonjwa kwa muda mrefu sasa, shida za kimawazo, vidonda vya tumbo na ata shinikizo ambazo ziliweza kumba maisha yake,

“Aliweza kujifungia kwa nyumba kwa siku kadhaa bila kula, kwa kweli alipambana na matatizo ya akili na mawazo,” Alielezea mmoja wa familia.

Msanii mmoja mbaye alianza kazi ya usanii wakati sawa na Kantai aliweza kuandika maneno yafuatayo kwa kimombo katika mtandao wake wa kijamii.

Chris Kantai

MC Sharon aliandika na kusema,

“THE SUN SETS YET AGAIN ON ANOTHER KENYAN SUPERSTAR AND TRAILBLAZER CHRIS KANTAI. GUTTED IS AN UNDERSTATEMENT GIVEN THE DEEP HISTORY WE HAD IN THIS RAP GAME AND ALSO AS VERY CLOSE FRIENDS.” MC Sharon aliandika.

Habari hizo za kifo chake kiliweza shtua watu wengi, katika rambirambi zake aliweza kuongeza nakusema kuwa ilikuwa baraka kupatana na msanii huyo,

Na pia aliweza mshukuru kwa mchango wake katika usanii wake.

“My biggest regret is not reaching out sooner like we had planned and being there for you when you must have needed it because life took us to different places and spaces,

“You were proud just like myself and was never one to cower in the face of adversary or ask for help randomly but that is that Maasai spirit and I am saddened no less at your timely demise.” Aliandika Sharon.

Akimalizia katika rambirambi na jumbe zake aliweza kumalizia na kusema kuwa kama vile watu wengi wanaishi na kumbukumbu zake ata yeye pia ataweza kuishi na kumbukumbu hizo.

Aliweza kumpongeza na kumwambia kuwa anajua alianza usanii mzuri na aliweza kufanya bora bali aliweza kusaulika mwishoni.

“Rest in power my G and say hi to 2pac and Biggie for me. That heavenly hip hop symphony just got more litty.” Sharon alisema.