Wawili kwa saba walioshikwa wiki jana kwa ajili ya kuiga sauti ya rais Uhuru na kisha kumlaghai mwanabiashara Naushad Merali waliweza kusema kuwa maisha yao yamo hatarini kwa sababu wasizozijua.
Joseph Waswa na Isaac Wajecheke jana walisema kuwa watu wanaoshukiwa kuwa polisi waliweza kuwafuata kwa kina na kisha kuwafuata waliweza kusema kuwa hawana nia mzuri kuhusiana na maisha yao.
“Kuna gari limekuwa ikija nyumbani mwangu Karen majira ya jioni na kuwa na watu ambao hawajulikani,ambao wanashukiwa kuwa ni polisi,” Waswa aliambia vyombo vya habari jana.
Wawili kwa saba walioshikwa wiki jana kwa ajili ya kuiga sauti ya rais Uhuru na kisha kumlaghai mwanabiashara Naushad Merali waliweza kusema kuwa
Waswa alisema kuwa ni kwa bahati mbaya kwa maana ameanza kufutwa bado kesi ikiwa mahakamani.Wawili hao na wenzao waliweza kushtakiwa kwa kulaghai watu na kisha kumdanganya Merali kuwa watamuuzia shamba iliyo maeneo ya Milimani kaunti ya Nairobi.
Waliweza kudaiwa kuwa walitenda kitendo hicho mnamo Januari 24 hadi Februari 1 wakiwa katika maeneo ya benki ya prime river side.
Raila explained why church returned Ruto’s brand new Mitsubishi Pajero
WAliweza kuwachiliwa wiki jana kwa dhamana ya 100,000 kwa kila mmoja na mahakama kuamuru waweze ripoti kila ijumaa katika ofisi ya DCI.
Mshukiwa huyo alisema afisa wa polisi wa DCI anayefahamika kama David Omore ameweza kumtishia maisha na kisha kumuambia kuwa ataweza kumuua.
“Kila mmoja huchukuliwa si mkosefu hadi pale ataweza kuthibitishwa ana hatia,nina shangaa sana kuwa afisa huyu anashinda kunitishia kuniua,
“Ameshinda kuniambia kuwa ameandikwa na ikulu ili aweze kuniua,” Alisema Waswa.
Waswa alisema kuwa polisi huyo ni mmoja wa walio mkamata na kisha kuenda nyumbani kwake Karen kuchunguza nyumba yake.
Pia alisema kuwa waliweza kuchukua shillingi 190,000 kutoka kwa mke wake ambaye ana uja uzito na kisha kuchukua shillingi 100,000 kutoka kwake.
Meet DP William Ruto’s pilot, Captain Mario Magonga (Photos)
Mshukiwa huyo aliweza kusema kuwa polisi huyo aliweza kumtesa pamoja na wenzake na anataka haki kutendeka.
Siyeyeye tu aliweza kuitishwa pesa pia mwenzake Wajecheke aliweza kuitishwa shillingi 50,000 na Simiyu kuitishwa 47,000
“Tulitarajia polisi huyo kuchukua pesa hizo kupitia OB,kama baadhi ya mali zetu bali alianza kututesa ili tuweze kumpa pesa hizo,” Waswa alieleza.
Mshukiwa huyo pia aliweza kuwashtaki polisi kwa kuchukua hati miliki za nyumba zake zote na kisha kuenda kuwasumbua wapangaji wa nyumba zake.
Aliweza pia kanusha madai kuwa yeye ni mlaghai kisha kusema yeye ni mwanabiashara maarufu anyejulikana.
Readmore:



