Thursday, 10 September 2026
Kenyan Digest

Margaret Wajobi asimulia vile aliweza pitia operesheni mara kumi

2 min read
Published 4 March 2019

Margaret ni mwanamke ambaye ameweza pitia changamoto nyingi maishani kisha baadaye akaweza kupata nguvu na ujasiri wa kupingana na changamoto zake.

Margaret Wajobi ambaye anajiita mama Precious na Hope aliweza kupitia operesheni kwa mara kumi huku watoto wake wakifariki baada ya muda mfupi.

“Baada ya kumaliza darasa la nane niliweza kuletwa Nairobi ili kumsaidia jamaa wa nyumbani,kwa sababu wazazi wangu hawakuwa na pesa za kunipeleka shule ya upili,

“Niliweza kupatana na kijana mmoja nikiwa na miaka 16 na kisha akanitia uja uzito huku nikiwa na shida ya mimba ya fumbatio(ectopic pregnancy),” Alieleza Margaret.

Baada ya kufanyiwa operesheni hiyo aliweza kukosa mtoto kwa miaka tatu,baada ya kukosa mimba aliweza kuwa na ujauzito tena huku mimba yake ikitoka moja baada ya ingine kwa mara nne.

“Baada ya mimba yangu kutoka niliweza kupata mimba ingine nikafanyiwa operesheni,kisha madaktari wakaniambia mtoto wangu ni mgonjwa,

“Nyama zake za ndani za tumbo zilikuwa zote nje na hakuwa na ngozi ya kufunika,aliweza kuekwa ngozi ya plastiki lakini kisha akaaga dunia baada ya miezi minne,

“Kisha baada ya mwaka mmoja niliweza kubeba mimba ingine kisha nikakua na shida ile na nikaenda kufanyiwa operesheni mtoto mimba ikiwa na miezi nane kama ile tu ingine,”

“Nilipozaa niliambiwa mtoto ana shida ya kupumua kisha akafariki baada y6a siku mbili,” Margaret alisimulia.Margaret ni mwanamke ambaye ameweza pitia changamoto nyingi maishani kisha baadaye akaweza kupata nguvu na ujasiri wa kupingana na changamoto zake.

Margaret aliweza kuolewa mara mbili huku wanaume hao wakimrudisha nyumbani kwao kwa sababu ya shida ya operesheni.

Katika ndoa yake ya mwisho mama mkwe aliweza kumfukuza siku tatu tu baada ya kufanyiwa operesheni kisha mtoto kuaga dunia,aliweza mleta mwanamke ambaye  angependa kuolewa na mume wake.

“Nilichapwa sana baada ya siku tatu za kufanyiwa operesheni,huku mama mkwe akikuja na mwanamke mwingine katika boma,

“Nilikatwa katwa na visu kwenye mikono yangu,baada ya kunichapa niliweza kupelekwa polisi nikaenda kufungiwa huko,

“Nyama zangu za ndani zilikuwa tayari zimetoka nje mahali nilikuwa nimefanyiwa operesheni,” Alizungumza Wajobi.

Ni masaibu ambayo aliweza kukumbana nayo na kisha kuamua kuwalea watoto wake wawili akiwa peke yake.