Connect with us

General News

Mtangazaji Mutahaba kufariki akipokea matibabu Afrika Kusini

Published

on


Ni machozi na kifo kilicho wakumba familia ya mtangazaji maarufu Ruge Mutahaba, hii ni baada ya kumpoteza mwanahabari huyo akiwa katika matibabu nchini Afrika Kusini.

Mutahaba aliweza kupumua pumzi yake ya mwisho Jumanne akiwa katika hospitali moja mjini Afrika kusini.

Mwanaume kumkatakata mke wake na kuchoma mwili wake

Mtangazaji huyo maarufu alikuwa mwelekezi wa kipindi cha mikakati na mipango ya maendeleo (strategy and programme development) katika runinga ya Cloud Media Group.

Aliweza kufariki baada ya kupambana na ugonjwa wa kushindwa kwa figo kwa muda mrefu.

Ruge Mutahaba

Ndugu yake Ruge aliweza simulia kifo chake alisema kuwa ilipotimu saa 04:30 masaa ya Afrika kusini, ndugu yake hakuweza kuona jua wala kuona watu tena pia kimya kilizidi kwa kufariki kwake.

“Leo ameweza kuamka akiwa hayuko sawa, daktari na watu wengine waliweza kumsaidia Mutahaba kwa njia mbalimbali, lakini mnamo saa kumi unusu masaa ya Afrika kusini aliaga dunia,

“Aliweza kufariki akiwa na viongozi wa dini na mdogo wake akiwa katika hospitali hiyo,

“Marafiki, familia wameweza kutuma rambirambi zao na kuwasili katika maeneo haya, kwa sasa familia inashukuru witikio wa watu waliofika hapa kutufajiri kwa muda mfupi,

“Utaratibu wa kuangalia namna za kumrudisha ndugu wetu nyumbani zinaendelea, ratiba rasmi ya msiba na mazishi itatolewa hivi karibuni,” Alisimulia Mombeki.

Hasira! Wananchi kuchoma gari la polisi kufuatia ajali ya barabara

Ni mwanahabari ambaye ata salia katika kumbukumbu za watu wengi hasa vijana wa nchi ya Tanzania kwa ukakamavu wake na ujasiri wake Ruge.

Ruge Mutahaba
Ruge Mutahaba

Wakati habari za kifo cha punde chake mwanahabari Ruge Mutahaba ziliweza kusambaa sana katika mitandao ya kijamii watu wanaofahamika na watu maarufu waliweza tuma rambirambi zao.

Rais John Pombe Maghufuli aliweza tuma rambirambi zake kwa familia kupitia mtandao wake wa kijamii wa twitter na kusema..

“I have received with shock information about the death of Ruge Mutahaba,” Aliandika Maghufuli. Aliweza kumjulisha Mutahaba kama kijana wake.

Haikuchukua muda mashabiki wasanii na marafiki zake waliweza pia kutuma rambirambi zao kupia mtandao huo.

@MariaSTsehai: Rest in peace our brother Ruge…Your contribution to the media industry has left an indelible mark!Pumzika kwa amani.

 

 

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending