Connect with us

General News

Mume wangu alikuwa na tabia ya kuficha nguo za wanawake chini ya kitanda

Published

on


PATANISHO: Mume wangu alikuwa na tabia ya kuficha nguo za wanawake chini ya kitanda

Felix alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Alice.

“Kuna mwanadada mmoja alinipigia simu asubuhi mda wa saa moja kabla sijaamka, akiniuliza kama nilimkosea. Sasa niliporudi jioni baada ya kazi nikapata mke wangu ameondoka na kubeba kila kitu na kutoweka.” Alisema Felix akiongeza, hapo mke wangu alikasirika na hivo ndio alitoka na akaondoka.”

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka mitano na wamejaliwa na watoto wawili ambao alienda na kuwaacha kwao.

Alipopokea simu yetu, bi Alice alisema kuwa mumewe ndiye alikuwa anamkanya maneno ya kuzungumza kwa redio na sasa yeye ndiye amempeleka redioni.

“Wewe ndio ulikuwa unaskiza hicho kipindi ukisema hakuna siku utawahi kanyanga redio jambo, how comes leo umefika huko?” Aliuliza.

Yenye umenitendea yote, four good years nimevumilia kwako na ndoa yangu na nikakupa maisha yangu tu yote na ukaichezea halafu sahii unanianika.

Ulishindwa kufika nyumbani ndio uniombe msamaha, sahii unaenda kwa redio. Na yenye umenitishia yote utanifanyia ukinipata si nilikupa ruhusa ufanye kile unataka?” Aliongeza Alice mwenye hasira tele.

Alice alisema kuwa mumewe ana tabia ya kuleta wanawake kwake kila anaposafiri na akirudi anapata nguo za wanawake chini ya kitanda.

Kwa hasira zaidi alifichua kuwa tayari ameolewa na anaomba Felix atafute mke mwingine.

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending