Nabii David Owuor amepatikana katika matata ya kunyakua mali ya familia ya billioni 1.5 katika eneo la Westlands kaunti ya Nairobi.
Familia hiyo imetuhumu nabii huyo ‘Mightiest prophet’ na kanisa lake la (Repentance and Holiness Ministry) kwa kunyakua mali kwa lazima katika barabara kuu ya Rhapta Westlanda na ingine katika eneo la Riverside.
Waziri Rotich mikononi mwa DCI kwa ajili ya kashfa ya mabwawa
Jana jamaa wa familia wa mwanamke huyo wa mali hizo walisema kuwa nabii huyo aliweza kumpokonya kupitia mpango ulioanzishwa 2005.
Waliweza kumtuhumu Owuor kwa kusema kuwa alizidi kuchukua mamillioni ya pesa kutoka kwa kodi ya majumba hayo makubwa.
Millioni ambazo zimeweza kusaidia Owuor kuendeleza na huduma yake ambayo imejulikana kwa sana na watu wengi nchini kote.
Photo Of The Day: Rashid Echesa officially hands over to Amina Mohamed
Katika mioyo ambayo imeteseka,walisema kuwa Owuor pamoja na mkubwa wa askofu katika kanisa lake waliweza kumdanganya mwanamke huyo anayefahamika Jayne Muthoni aweze kuchagua wafuasi wa Owuor.
Lily Njage kama msaidizi wa mwelekezi katika Shaba Investment Limited,na kumsajili kama mwenye nyumba hizo.
Ili waweze kuchukua na kudhibiti mali hiyo kutoka mikononi mwa Owuor, jamaa hao walidai kuwa Jayne Muthoni hakuwa timamu alipomsajili Njage awe maneja wa mali zake.
Waliweza pia kudai kuwa Muthoni alikuwa ameoshwa ubongo na kupewa dawa zisizo julikana na kusababisha Muthoni kupoteza akili yake.
“Tunataka mali ya dada yangu iweze kurudishwa, walimlazimisha dada yangu Jayne Muthoni aweze kuchagua msaidizi wa mwelekezi ili waweze kuchukua na kudhibiti kampuninna mali zake.
“Wamemuibia, kuna shughuli ambazo niliona zimefanyika za millioni mia saba, waliweza kutoa pesa kwa benki ya dadangu,” Alisimulia ndugu yake Muthoni Duncan.
Mary Wambui Murder: Kucheleweshwa kwa dhamana ya washukiwa
Duncan aliweza kuongoza familia hiyo hadi katika mali ya Muthoni ilikokuwa eneo la Riverside ili waweze kupewa mali hiyo, haikuwa jambo la ajabu bali waliweza kupata kuwa nabii huyo aliweza kuhamia katika moja ya nyumba za Jayne Muthoni.
Na kuifanya kama ofisi ya kanisa yake.



