Ndege za Nairobi zilizokuwa zimepangwa kutua katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta(JKIA) zimeweza kuamua kutua Mombasa na ata zingine kuenda nchi ya Tanzania.
Hii ni kufuatia mgomo wa wafanyakazi ulioanza mapema jumatano, na kuacha abiria wengi wakiwa wamekwama katika uwanja huo tangu usiku wa manane.
Nabii Owuor kutuhumiwa kwa kuchukua mali ya billioni 1.5
“Tuna washauri abiria wote ambao wanatumia ndege ya Nairobi ya JKIA, waweze kuwasiliana na watu husika wa ndege ili kudhibitisha wakati wa usafiri wao, na mipangilio ya usafiri.” Mamlaka ya Kenya Airport walisema katika kauli.
Baadhi ya abiria waliweza kulalamika katika mitandao ya kijamii, kuhusu kukatizwa kwa ndege zao na hata kukaa kwa muda mrefu katika uwanja wa ndege bila hatua yeyote kuchukuliwa.
Zifuatazo ni baadhi ya lalama za abiria na wasafiri walizoziandika katika mitandao ya kijamii;
PATANISHO: Kama unanitaka you know what to do!
“I was to have morning flight to Oslo from JKIA this morning , now heading to Tanzania….,” Jacob Abere Matlala aliandika.
“This is an International Airport, We are showing a very bad picture and other Airports are benefiting from this, Ethiopia, Uganda and Tanzania. What the police are doing it’s even worse,” Sam alisema katika mtandao wake wa twitter.
Wengi wameweza kushtumu mgomo huo na kusema kuwa uwanja huo wa ndege ni wa kitaifa, na wengi kusema kuwa wangeweza kuwaunga mkono wafanyakazi hao.
Polisi na kitengo cha (GSU) wameweza kupigana na kupambana na wafanyakazi hao na kuwalazimu kuweza kufyatua vitoa machozi.
Huku wakimkamata katibu mkuu wa KAWU Moses Ndiema akikamatwa na polisi na kisha kutiwa ndani.
Gari la maji ilionekana ikiwasili katika eneo hilo la mgomo na pia gari za abiria kukatazwa na kuzuiwa kutumia barabara hiyo ya JKIA.
Foleni refu na abiria kukaa chini katika maeneo ya kuwasili inaonyesha hali ilivyo katika eneo la uwanja wa ndege wa JKIA,wasimamizi wa JKIA waliweza kuzungumza na abieia wao kupitia kauli katika hali hiyo.



