Connect with us

General News

Nilitoroka kwangu kwani niliogopa watoto wangu watanipiga

Published

on


PATANISHO: Nilitoroka kwangu kwani niliogopa watoto wangu watanipiga

Bwana Charo aliomba apatanishwe akidai mkewe bi Edith, aliondoka baada ya wawili hao kukosa kuelewana akidai kuwa shetani aliingilia kati ndoa yao.

“Huyu bibi mimi nilikuwa nampenda sana lakini sasa kadri tunapoishi, unajua shetani ana majaribio yake. Huyu shetani alinichezea mchezo ambao sio lakini ashindwe!.” Alijieleza.

Bwana Gidi huyu mke wangu tulikuwa tunaishi Mombasa na nikimwambia twende kwetu nyumbani Mariakani huwa hakubali, lakini kwao hupenda kwenda kila baada ya mwezi miwili. Sasa ikabidi saa zote akienda namwambia sipendelei.

Siku moja nikamwambia hivo vyenye wewe huenda wewe baki huko nitakufuata, yeye akaniambia hata asubuhi nitamwona amefika huko. Sasa aliporudi mimi nikamchapa. Sasa nikitaka kumchapa nikakumbuka ana vijana wakubwa na nikaogopa watanichapa na nikatoroka.

Mke naye akakaa Mombasa nami nikarudi Nairobi na hatujakuwa tukizungumza hata kiasi.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka ishirini.

Alipopigiwa simu bi Edith alisema kuwa aliskia kutoka kwa dadake Charo kuwa alikuwa amefunga ndoa mara mbili huku akidai kuwa haoni wawili hao wakirudiana.

“Kurudiana sioni kwani nitakuwa naingilia nyumba nyingine ya bibi wa pili. Msamaha nilikusamehe kitambo sana na nikakuacha uishi maisha yako mimi niishi yangu.” Alisema.

Pata uhondo kamili.

 

 

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending