Thursday, 10 September 2026
Kenyan Digest

Tarehe na siku ya mazishi ya msanii Chris Kantai kupangwa

2 min read
Published 5 March 2019

Chris Kantai ni msanii ambaye aliaga dunia kutokana na shida ya vidonda vya tumbo, mashabiki na wasanii wengi wameweza kungoja kwa hamu siku ya kuzikwa kwake.

Huku tarehe na siku ya kuzikwa kwa msanii huyo ikipangwa na kusemekana kuwa ataweza kuzikwa Ijumaa.

Kulingana na aliyekuwa msanii, Buddha Blaze alisema kuwa marafiki, familia na mashabiki wataweza kuwa na mkutano wa kupanga jinsi ya kumzika msanii Kantai na pia jinsi ya mipangilio ya muziki siku hiyo.

R.I.P: Kantai kuaga dunia baada ya kulazwa hospitali kwa siku mbili

Familia imeweza kutoa namba ya kutoa mchango kwa ajili ya mazishi hayo, (paybill no.8913000) jina la akaunti ikiwa ni la marehemu Kantai.

                        Chris Kantai

Wameweza kupeana namba hiyo kwa ajili ya wasamaria wema watakao jitokeza na kumchangia Chris Kantai, na kwa sababu ya kukamilisha mipango ya mazishi hiyo.

“Familia yake inaomba msaada wako,l eo kutoka saa kumi na moja jioni familia, marafiki, mashabiki wataweza kuwa na mkutano katika eneo la Gracia Garden ili kuweka ratiba kwa ajili ya mazishi.

Kantai alikuwa na mashabiki wengi na pia nyimbo zake zilipendwa kwa sana lakini hana chochote cha kuonyesha alikuwa maarufu,” Alieleza Buddha.

Murder!! Mabawabu watano kuuwawa Kilingili kaunti ya Vihiga

Msanii Kantai aliweza kufariki wiki jana jumatano akiwa anatibiwa katika hospitali ya St Francis aneo la Kasarani kisha akaweza kukata roho kwa muda usiokuwa mrefu.

Chris Kantai

Baadhi ya nyimbo za Kantai ziliweza kuenea kwa sana, mara yake ya mwisho kutoa wimbo ilikuwa mwaka wa 2016 huku akiwa ana mshirikisha Khaligraph.

Aliweza kuimba wimbo wake mmoja akimshirikisha STL, huku STL akiandika majuto yake ya kutomuona Kantai alipokuwa mara ya mwisho nchini.

Wakenya kuomboleza kifo cha muigizaji wa kipindi cha ‘Selina’ Kone

Akiandika katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram alisema kuwa alipoingia katika sekta ya usanii Kantai ndiye alimshika mkono na kumuamini kuwa anaweza kazi ya usanii.

Aliongeza na kusema kuwa alipoanza usanii mwaka wa 2005 Kantai alimshika mkono wakati kila mtu alikuwa amemtupa mbali kwa sababu hakuwa amejua sana.

Kantai aliweza kufariki akiwa na zaidi ya miaka 40.