Huwa wanaendesha gari za dhamana na pia wao si kidogo pia wanavaa mavazi ya pesa ili kuweza kuwalaghai watu wengi.
Mwishoni mwa wiki walijua kweli hawakukosea waliposema siku za mwizi ni arobaini, walaghai hao saba waliweza kukamatwa na DCI huku wakiwa wamewalaghai watu dhamana ya pesa.
Model who put her virginity up for sale secures multi million offer from Japanese politician
Huku wakiwadanganya kuwa wana mipango ya zabuni katika ofisi ya rais Uhuru Kenyatta, hawakuweza kushtakiwa bali waliweza kuwekwa rumande kwa wiki mbili ili DCI aweze kumaliza uchunguzi wake.
Walaghai hao wanachunguzwa kwa kuhusika katika kuwadanganya watu na kuwanyanganya pesa pia kujifanya kuwa wao ni viongozi katika ikulu na kuwa wana zabuni ambayo wanataka wenye pesa hao wahusike nayo.
Kundi hilo lina kiungo cha ofisi ya ikulu, Harambee house na maofisi kubwa ambayo huwa wanatumia ili kukamilisha ulaghai wao.
Walaghai hao huwa wanawadanganya wanabiashara ambao ni tajiri huku wakiwaambia kuwa wana zabuni kubwa sanasana ya kutoa bidhaa.
‘Fake president Uhuru’ amlaghai mwanabiashara millioni 80 – Polisi
Wanahabari wa DCI walisema kuwa Naushad Merali mwentekiti wa kampuni ya Sameer alikuwa bado hajarekodi kauli kwa maana alikuwa nje ya nchi huku mdogo wake anayefahamika ka bwana Gitonga aliweza rekodi kauli kwa ajili ya jambo hilo.
Polisi walisema kuwa Merali ataweza andikisha kauli yake atakapo rudi nchini wiki hii.
Usiku wa jana mnenaji wa ikulu aliweza kukataa kuhusu kauli hiyo “Sina kauli kuhusu jambo hilo,” Kanze Dena aliambia gazetti la star.
Ilikuaje: Cashy aeleza kilichomfanya atengane na mume wake Khaligraph
Gilbert Kirunja, 33, aliweza kukamtwa na pia katika amehitimu shahada ya IT na pia niyeye ambaye aliweza iga sauti ya rais Uhuru Kenyatta.
Wachunguzi wa DCI waliweza kupigwa na butwaa baada ya kuenda kufanya uchunguzi katika nyumba yake anayoishi Kirunja eneo la Karen.
Polisi walisema kuwa nyumba ya Kirunja ni ya kifahari huku vyumba vya kulala vikiwa kumi, pia Kirunja ni yeye huwa anawaambia walaghai hao watakavyo fanya.
Mnamo tarehe 14 Januari Kirunja aliweza kumpigia Merali simu huku akiongea kama rais na kisha kumuambia zabuni ya ikuli ambayo anataka kampuni ya Sameer iwe miongoni mwa watakao kuwa katika zabuni hiyo.
Merali hakuweza kutofautisha sauti ya Kirunja na rais kwa maana alikuwa anaongea sawa na rais.
Mpango huo ulikuwa mzuri sana, kwamba ‘rais’ alivyomwambia Merali atume millioni 10 ili kufanya mipango ya masuala ya vifaa. Baada ya dakika 30 wanaume ambao walikuwa wamevalia mavazi ya pesa na kuingia katika kampuni ya Sameer waliweza kuwasili na kuenda katika ofisi ya mwenyekiti Merali.
Waliweza kumuambia wametumwa na rais kuchukua pesa na kisha akawapa na kuenda, walaghai hao ambao walikuwa wanatumia 0722208842 kumpigia Merali kuhusu zabuni ya ikulu ndipo alipojua ni walaghai ambao waiga sauti ya rais.
Hii ni baada ya kushinda wakimpigia simu na kumuambia aweze kutuma pesa za zabuni hiyo.



