Connect with us

General News

Bwana yangu amekua kama makanga, anasonga na kila mwanamke

Published

on


Jose alituma ujumbe akisema amekosana na mkewe wa miaka kumi na mitano baada ya kuenda nje ya ndoa na wamekosana ingawa wanaishi pamoja. Aliongeza kuwa hakuna imani na upendo mwema kwa ndoa.

“Nilianza kutongoza tongoza wanawake wengine lakini niliwachana na huyo mwanamke miaka minne iliyopita na mke wangu hajawahi sahau hayo mambo. Hayo mambo hata yalisababisha mimba mbili kutoka.” Alielezea bwana Jose.

Wawili hao wana watoto watano.

Kwa hivyo hautawahi rudia? Huo ni uwongo, vile wewe unakaa kama gari kila stage unasimama. bi Vivian alimpasha baada ya kuskiza akiomba msamaha.

Ni nini ulikosa yenye ikafanya uni double deal na wanawake wengine?. Nataka uambie kina Gidi kama ni Mombasa raha ilikuwa shida kwani nilikuvumilia hadi ukawa mwenda wazimu, watoto nilikuzalia lakini bado huridhiki.” Aliongeza Vivian huku akiwa na wingi wa machungu.

Isitoshe aliongeza kuwa mumewe aliwahi rukwa na akili na akamuombea na akapona na licha ya kuingia kwa ndoa bila chochote, mumewe alikuwa anapitisha wanawake wengine kwa jiko lake na kulalia kitanda chake.

Alikubali kumsamehe lakini yuko tayari kumuacha akirudia tena.

Pata uhondo kamili.

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending