Tuesday, 8 September 2026
Kenyan Digest

Watu wanne kufariki na 16 kujeruhiwa katika ajali ya barabara Narumoru

1 min read
Published 21 January 2019

Saa tano usiku wa kuamkia leo watu wanne walifarki na 16 kujeruhiwa katika ajali ya barabara Narumorutu.

Wanne hao walifariki kupitia ajali ya barabara iliofanyika katika maeneo ya narumoru kaunti ya nyeri.

Basi ya watu 45 ya kampuni ya (Northern E-coach Sacco), ilikuwa inasafiri kutoka Nairobi kuelekea Isiolo na lori iliyobeba watu watano lilikuwa linasafiri kutoka Meru kuelekea Nairobi.

Mkuu wa polisi wa kaunti ya Nyeri Fredrik Shisia alithibitisha tukio hilo  kisha kutangaza kuwa watu 16 walijeruhiwa kutokana na ajali hiyo.

Dereva wa basi hilo aliripotiwa kupata majeraha mabaya, katika waliofariki polisi wawili waliokuwa wakiwasindikiza dereva na raia walipoteza maisha yao kupitia ajali hiyo.

             SEE THE PICTURE BELOW

Polisi wanaamini ajali hiyo ilisababishwa na magari hayo kugongana ana kwa ana, waokoaji walibidi kukata lori hilo la G4s ili kuwaokoa abiria waliokuwa wamekwama ndani ya magari hayo.

Waathiriwa wa ajali wanaendelea kupata matibabu katika hospitali mbalimbali pamoja na hospitali ya rufaa ya nyeri, hospitali ya nanyuki ambayo haiko mbali na eneo la uhalifu.

SEE THE PICTURE BELOW

Pia polisi watarajiwa kupeana habari  kuhusu ajali hiyo wakiwa bado wanakusanya uchunguzi zaidi, magari hayo yamepelekwa katika kituo cha polisi cha Narumoru, inakuja siku moja baada ya watu sita kufariki katika ajali ingine kutokea katika barabara ya Olkalou iliyohusisha matatu ya abiria 14 na lori.