Wednesday, 9 September 2026
Kenyan Digest

Afisa wa kliniki katika hospitali ya Chesongoch apigwa risasi Marakwet Mashariki

1 min read
Published 24 January 2019

Milio ya risasi na umwagaji wa damu ndio umekuwa mtindo wa wananchi wa Kenya wiki mbili zilizopita.

Katika maeneo ya Marakwet Mashariki, afisa wa kliniki alipigwa risasi hadi kufa na majambazi katika barabara ya Tot-Chesongoch Marakwet Mashariki.

David Kipchumba clinal officer

Marehemu David Kipchumba Kipkore, wa miaka 29, alikuwa anaendesha pikipiki na watu wengine wawili walipo pigwa marisasi katika eneo la Chekumutet karibu na kituo cha Kaokobil.

Alikuwa afisa wa kliniki katika hospitali ya ujumbe ya Chesongoch.

Mkuu wa afisa Vincent Kitili wa maeneo ya Marakwet Mashariki alisema abiria mmoja Julius Kilonzo alipata majeraha ya risasi kwa mguu wake na mwendesha pikipiki Titus Kibet, dereva wa miaka 23,  hakuweza kuumia pahali popote.

“Mashambulizi hayo yalifanyika jana usiku na tumetuma maafisa,ilikuchunguza waliousika katika mauwaji hayo,”Kitili alisema.

Mwili umepelekwa katika chumba cha kuifathi maiti cha Tot.

Kitili aliamurusha magari ya abiria safiri Tot-Chesoi-Kaosowary na Tot-Arror watakuwa wakisindikizwa na polisi kuanzia leo.

Mvutano wa eneo hilo uko juu katika maeneo hayo na polisi wanashika doria katika njia nyingi.

Mashambulio yana shukiwa kufuatia kauli ya mwisho iliyotumiwa na sehemu ya wazee walio omba kurudishwa kwa mifugo 82 walilalamika mifugo hiyo iliibiwa Marakwet kupitia eneo la Kotuut.

Read More Here