Wednesday, 10 June 2026
Kenyan Digest

Ashtakiwa kwa kumtwanga aliyekuwa mke wake siku za nyuma – Taifa Leo

Staff
1 min read
Published 30 April 2022

Ashtakiwa kwa kumtwanga aliyekuwa mke wake siku za nyuma

NA RICHARD MUNGUTI

MUME aliyemchapa mke waliyetengana ameshtakiwa mahakamani.

Jaylan Mwaniki alishtakiwa mbele ya hakimu mwandamizi Derrick Kutto kwa kumshambulia na kumuumiza Barbra Vugutsa katika kijiji cha Mathonge eneo la Waithaka kaunti ya Nairobi mnamo Machi 14.

Hakimu alifahamishwa kisa hicho kilitokea mwendo wa saa 11 alfajiri.

Mshtakiwa alimshambulia Vugutsa alfajiri alipofungua nyumba na kumpata akimvizia nje ya nyumba.

Mshtakiwa aliingia ndani ya nyumba na kuanza kumnyeshea makonde na masumbwi.

Vugutsa aliponyoka na kutoroka lakini Mwaniki akamfuata unyounyo.

Wananchi walimwokoa Vugutsa.

Mahakama ilimwachilia mshtakiwa kwa dhamana ya pesa taslimu Sh20,000.

Salah na Kerr waibuka wachezaji bora wa tuzo za Shirika la...


About the author