Askofu wa kanisa la calvary alitoroka jumapili kanisani kabla ya kuona kizaazaa ili kujificha wanachama wanao dai alikula pesa zao. Wanachama hao waliwasili kanisani wakihitaji akiba yao.
David Ngari almaarufu(Gakuyo)ni mwenye chama cha Ekeza akiba (Ekeza Akiba and credit cooperative society).
Wanachama walisema kuwa walituma uondoaji wa pesa mwaka2017 baada ya fununu kuwa chama hicho kunaanguka kwa sababu ya udanganyifu.
Waliwasili katika kanisa la Ngari wakidhani watampata ilhali hawakumpata ili awaeleza lini ata wapa pesa zao.
Lakini Ngari alikataa kuzungumza nao na kuenda na gari wasilolijua baada ya misa ya jumapili. Wanachama walidai kuwa Askofu huyo alitumia pesa zao kujidumu katika kampeni yake mwaka wa 2017.
Alipokuwa akiwania kiti cha ugavana kaunti ya kiambu, baadae askofu Ngari alijitoa katika kinyang’anyiro hicho akidhani kuwa (formed united kiambu movement) itamshika mkono lakini ikashika mkono gavana Ferdinand Waititu.
“Tuliweka akiba katika chama kwa ahadi nyingi za kimaendeleo pamoja na kupata shamba kwa bei rahisi,”Benard Irungu alisema.
Alisema alikuwa na kiasi cha shillingi 285,000 katika akiba ambazo ziko na chama hicho na alikuwa ameonelea kumpeleka kortini.
Aliomba chama shillingi30,000 na zikakataliwa alipo amua kutoa akiba zake.
“Niliomba kutoa akiba yangu mwaka 2017 Januarinikaambiwa ningije siku 60 za kufanya kazi lakini hadi sasa hawajanipa pesa zangi,” Irungu aliongezea.
George Njuguna ambaye hawezi lipia watoto wake karo ana akiba ya shillingi 282,000 katika chama hicho.
“Nilijiunga na chama hiki kwa sababu Ngari ni mtumishi wa mungu nilijihisi kuwa pesa zangu zitakua mahali pazuri,”Njuguna alisema.
Mwendeshaji wa pikipiki Robert Mathenge ameweza kuweka shillingi 95000 baada ya kupewa ahadi kuwa atapata shamba katika mojawapo ya mali za Ngari. Mathenge alisema kuwa hakupata shamba lolote ilhali ameweka pesa zake.
Ngari alipaswa kupeana kaulu jana kwa wanachama lakini hakuweza.



