Connect with us

General News

Baba mkwe alitishia kunipiga risasi

Published

on


Bwana Joseph alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Naomi ambaye walitengana na kwenda kwao.

Kulingana na Joseph ambaye anafanya kazi ya ulinzi usiku, yeye hurudi nyumbani asubuhi na hulala hadi saa nane mchana. Cha kushangaza ni kuwa kila anapoamka, mkewe huwa ameondoka na jambo hilo likamkasirisha sana.

Soma usimulizi wake.

Sasa tumeona kwa miaka miwili na tuna mtoto mmoja. Ilifika last year mwezi wa sita, nafanya kazi ya soldier na nilipotoka kazini nikamwambia achukue fedha za matumizi yake na mtoto.

Yeye anajua nikilala mimi hulala hadi saa nane, naye anatoka na mtoto. Siku moja tu nikajifanya nimelala na nikaamka mapema na sikumpata. Kumwuuliza amekuwa wapi nikamwambia arudi alikotaka kwani haniskii kama bwanake.

Sasa alifunganya virago vyake na kuondoka, babake naye akanitishia kuwa atanipiga risasi kwani yeye ni polisi. Isitoshe, babake nikama hakuwa anataka nimuoe kwani aliwahi muambia kuwa amemtafutia bwana mwingine polisi ambaye alitaka amuoe.

Kulingana na Joseph, wawili hao hawajazungumza miezi miwli tangu watengane lakini mara ya mwisho kuzungumza, mkewe alisema kuwa atafanya harusi mwaka wa 2023 na mwanaume mwingine.

Cha kushangaza ni kuwa nambari aliyopeana Joseph haikuwa ya Naomi bali ilikuwa ya Mary na wawili hao hawakuelewana.

 

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending