Wednesday, 10 June 2026
Kenyan Digest

Bunge la kaunti latoa msaada kwa shule ya umma – Taifa Leo

Staff
1 min read
Published 21 March 2022

Bunge la kaunti latoa msaada kwa shule ya umma

NA STANLEY NGOTHO

BUNGE la Kaunti ya Kajiado limefanikiwa kukusanya raslimali za kufadhili shule ya umma iliyokuwa haina vifaa muhimu vya shule.

Timu iliyojumuisha Spika Johnson Osoi na Bodi ya Bunge la Kaunti hiyo inayosimamia Utowaji Huduma, ilitoa ufadhili wa madawati 50 hatua iliyolenga kuashiria kuwa wafanyakazi wa Bunge la Kaunti, wanazidi kuhudumia jamii.

Shule ya Msingi ya Nkama iliyopo Wadi ya Illodokilani maeneo ya ndani ya Kajiado Magharibi ina walimu wawili pekee waliotumwa na Tume ya Kuajiri Walimu.


About the author