Katika kipindi cha dead beat na mtangazaji wako umpendaye Massawe Japanni, mama mmoja aliweza piga simu akiomba baba wa mtoto wake aweze kupigiwa simu na kufanya jukumu lake.
Susan Mutheu alisema kuwa aliweza kuwa na uhisiano na ndugu wa tajiri yake, aliyekuwa amemuajiri na kisha kumtia mimba mwana mke huyo na kukimbia majukumu yake.
“Nilipewa mimba na ndugu ya tajiri yangu, aliweza nipeleka kwao, na kisha nikatoka huko na kuenda kuzalia kwetu,nilizaa mtoto kijana,
“Tangu nilipomzaa mtoto huyo hajawahi nisaidia wala hajawahi muona mtoto huyo na sasa ana miaka mitano,” Alisimulia Susan
Najua Ben Githae ana watoto sita nje ya ndoa – Rose Wanjiru
Tajiri yake aliweza jua kuwa Susan ana uhusiano wa kimapenzi na ndugu yake huku akikosa kumshawishi mwanamke huyo.
Susan alisema kuwa walikuwa wanapatana nje na bali si kwa nyumba ya tajiri yake. Aliweza kusema kuwa anapompigia mwanaume huyo simu na kisha kusikia sauti yake huwa ana kata simu hiyo.
“Nina mpigia simu akisikia ni sauti yangu huwa ananikatia simu na hajawahi msaidia mtoto huyu tangu ni mzae,” Susan alisema.
Baada ya muda usiokuwa mrefu mwanaume huyo aliweza pigiwa simu bali hakudhubutu kuzungumza bali aliweza kukata simu.
Ruto aomba msamaha kwa ‘mavazi yasiyo faa’ katika tukio la mahakama
Ni shida na masaibu ambayo wasichana wengi wa kazi huwa wanapitia mara tu wanapowasili Nairobi kutoka mashambani, wanaume kuwatrumia tu kwa faida yao na wanapo beba mimba hawaonekani tena.
Susan aliweza kusema kuwa mtoto wake jana aliweza kutoka shule kisha kupita moja kwa moja kuchukua kamba ili aweze kujitia kitanzi.
“Jana niliambiwa na mama yangu kuwa mtoto wangu aliweza kutoka shule na kutaka kujitia kitanzi, alipoulizwa kwanini anataka kujiua alisema kuwa wanafunzi wenzake wana baba ilhali yeye hana,” Alizungumza Susan
Mashabiki waliweza kumuambia Susan aweze kupeleka mwanaume huyo kwa idara ya watoto ili aweze kuchukua jukumu lake kama baba wa mtoto wake.
Huku wengine wakisema kuwa mwanaume huyo aliweza kumtumia mwanamke huyo na kisha kutoroka tu.



