Wednesday, 9 September 2026
Kenyan Digest

Hali tatanishi ya kifo cha Lorraine Kerubo Ogoti aliyefariki Toronto Canada

1 min read
Published 24 January 2019

Familia moja katika maeneo ya Ongata Rongai ilipoteza tabasamu walipopata ripoti kuwa msichana wao amefariki katika hali tatanishi.

Sasa wanahitaji haki ifanyike ili waweze kujua kilichosababisha mtoto wao kufa na kutotimiza ndoto zake za maisha.

Kerubo alikuwa anaishi Toronto alipopatikana Jumanne katika hali maututi katika chumba kimoja kisha akafa baada ya muda mfupi kwa hali isiyojulikana.

Polisi waliotembelea maeneo hayo ya kitendo hicho walisema kuwa wanashuku mwanamke huyo alipigwa na mwanaume kisha akafa.

Lorraine kerubo Ogoti aliyefariki Toronto, Canada

Walielezea kuwa inawezekana kuwa kitendo hicho kinaeza kuwa kuuwawa ama kujiua, lakini swali kuu ni je ni kujiuwa ama nikuuwawa na mpenzi wake?

Baada ya kupokea simu ya 911 katika ghorofa hiyo mwathiriwa alipopatikana polisi na madaktari walipata Lorraine Kerubo Ogoti wa miaka 30 katika hali mbaya lakini baadaye akafariki.

Kulingana na ripoti tofauti, mwanaume aliyekuwa ametuhumiwa katika kitendo hicho alipatikana ghorofa ya chini nje pia akiwa na majeraha na pia akafa.

Uchunguzi wa maiti uliofanyika Jumanne, ulipata kuwa mwanaume huyo alikuwa anaitwa Mowlid Hassan na alikufa kwa sababu ya nguvu za kiwewe yaani (blunt force trauma).

Polisi wa Toronto wanao chunguza kisa hicho walisema kuwa hawataweza kutafuta washukiwa wengine kwa sababu hawaamini kuwa kama kuna washukiwa wengine ambao walikuwa ndani ya kisa hicho.

Hata hivyo polisi bado hawajapeana habari zaidi kuhusu hali ya kisa hicho cha mauji.

Ama uwezo wa uhusiano baina ya mwanaume na mwanamke huyo.

Mwili wa mwathiriwa utawasili katika kituo cha ndege cha Kenyatta hivi leo kwa matayarisho ya mazishi. Mama kerubo alisema kuwa mtoto wake alikuwa ameenda kusoma katika chuo kikuu.

Read More Here