Friday, 13 November 2026
Kenyan Digest

James Karanja asimulia jinsi alivyozaliwa akiwa huntha

2 min read
Published

James Karanja ni mwanaume ambaye alizaliwa akiwa huntha. Huntha ni mtu ambaye alizaliwa akiwa na sehemu ya kike na kiume pamoja.

Baada ya kuzaliwa, kulikuwa na taharuki katika kijiji chao kwa maana watu hawakuweza kuelewa yeye ni mtoto wa aina gani, huku akipelekwa kanisani ili aweze kuombewa na askofu.

Ilikuaje: Jacinta Wanjiku aeleza vile alivyoozwa na mama yake

“Askofu hakuelewa mimi ni mtoto wa aina gani kisha akasema niweze kupelekwa hospitalini kwa matibabu zaidi. Madktari pia waliweza kushindwa kunitibu ,na kisha wakasema niweze kulelewa kama msichana.

Tuliporudi nyumbani baba yangu aliweza kutoroka na kusema kuwa hajawahi ona jambo kama hilo katika kijiji chao.” Alisimulia James.

Baada ya muda usiokuwa mrefu, mama yake aliweza kutoroka na kumuacha kwa miaka sita kisha akaweza kurudi. James alipokuwa aki lelewa na nyanya yake aliweza kuitwa jina la kike, Mary Waithera.

Nilipomaliza darasa la nane, hapo ndipo palikuwa na changamoto kwani nilisomea shule la wasichana.

Nikiwa katika kidato cha kwanza siku moja niliweza kuamka usiku wa manane na nikaenda kuoga hapo ndipo niliweza kujua kuna utofauti katika mwili wangu.

Niliona sehemu ya siri ya mwanaume ikikuwa,mhapo ndipo niliweza kujielewa vizuri mimi ni nani.

Nilikuwa navutia wasichana sana na hata walikuwa wananitumia barua za kimapenzi hapo ndipo niliweza kufukuzwa shule kwa madai kuwa nimeleta uhusiano wa ngono shuleni.” James aliongea.

Ilikuaje: Mama yangu alibakwa kisha kuuwawa – Rose Nyabate

Aliweza kurudi shule na kisha kumaliza kidato cha nne. M

namo mwaka wa 2016 aliweza kujua kuwa hajabatizwa hapo ndipo aliweza kuitwa jina la James Karanja na kuacha jina ambalo alikuwa amepewa tangu alipokuwa mtoto.

Ni kisa ambacho kiliweza msababisha mama yake mzazi kupatwa na shida ya mawazo na kisha kumuathiri kwa sana na kuambiwa hawezi akapona.

Tuliweza kumpeleka hospitali ya Mathare bali tukaambiwa hawezi pona, mama yangu amekuwa akinilea na kunishika mkono mahali popote niliweza kuanguka,

Amenilea na kunipa msaada ambao nilihitaji.” Alizungumza James.

Changamoto kuu anayopitia ni kuwa katika vyeti vya kuzaliwa na vya shule ameweza kusajiliwa kama Mairy waithera bali katika kitambulisho amesajiliwa kama James Karanja.

“Nyanya yangu alikuwa ananiambia anataka niwe msichana mzuri ili niweze kuolewa na mwanaume wa maana, bali hisia zangu zilikuwa zinatofautiana sana na mawazo yao.” James alieleza.