Friday, 6 November 2026
Kenyan Digest

Kariobangi Sharks vs Everton: Everton wapondwa ugenini ▷ Kenya News

2 min read
Published

Timu ya Kariobangi Sharks, yenye ujasiri wa simba mnamo Jumapili, alasiri ya Julai 7 ilipambana na timu inayoshiriki katika ligi ya primia nchini Uingereza na kutoka nayo sare ya moja kwa moja katika mechi ya kihistoria iliyochezewa uwanja wa kimataifa wa kasarani.

Duke Abuya alifunga bao la ufunguzi katika kipindi cha kwanza kabla ya Joel Williams kusawazisha kwa faida ya Everton kutokana na mkwaju wa adhabu katika kipindi cha lala salama.

Habari Nyingine: Mwanakandanda mkongwe Joe Kadenge aaga dunia

Habari Nyingine: AFCON 2019: Benin waipiga Morocco 4-1 kupitia penalti baada ya kutoka sare ya 1-1

Licha ya timu zote mbili kupata fursa tele za kufunga mabao, wachezaji walibadhiri nafasi za kutia mpira kimiani, huku mechi ikimalizika kwa sare ya moja kwa moja katika muda wa kawaida.

Ilibidi uamuzi wa mwisho katika mechi hiyo iliyobainisha kutoshana kwa nguvu utolewe kupitia kwa matuta ya penalti ambayo mshindi alikuwa Kariobangi Sharks.

Habari Nyingine: AFCON 2019: Sadio Mane aisaidia Senegal kuikanyaga Uganda 1-0 na kuingia robo fainali

Wafungaji wa mabao ya muda wa kawaida Williams na Abuya wote walikosa kufunga panalti zao katika duru ya kwanza ya upigaji wa penalti ambapo Abuya alichapa mkwaju uliopaa juu ya lango.

Mkwaju wa Adeniran wa Everton uliokolewa na kipa Brian Bwire ambaye licha ya kuwa golikipa, baadaye alifunga mkwaju wa penalti ulioipa Kariobangi Sharks inayoshiriki ligi kuu ya soka humu nchini ushindi wa Kihistoria.

Sharks walijitengea miadi na Everton mapema mwaka huu baada ya kuitandika Bandari FC katika kinyang'anyiro cha Sportpesa Supercup kilichoandaliwa nchini Tanzania.

Wakati huo huo hii ilikuwa ziara ya pili ya Everton katika eneo la Afrika Mashariki baada ya timu hiyo kufanya ziara ya kwanza nchini Tanzania miaka miwili iliyopita.

Wakati huo walipambana na Gor Mahia waliokuwa mabingwa wa makala ya kwanza ya Sportpesa Supercup.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko News