Friday, 13 November 2026
Kenyan Digest

Mabawabu watano kuuwawa Kilingili kaunti ya Vihiga

2 min read
Published

Wananchi wa Kilingili kaunti ya Vihiga waliweza kuamka na mshangao mkubwa walivyo kumbana na maiti tano katika soko moja eneo hilo.

Majambazi waliweza kuwauwa mabawabu watano waliokuwa wakilinda duka za soko hiyo,wanachi hao wanaamini kuwa ni mauaji ambayo yalikuwa yamepangwa ili majambazi hao waweze kuuwawa.

Murder most foul: Magistrate linked to brutal murder of lawyer husband

Kisa hicho kilitendeka mwishoni mwa wiki huku kikiwaacha wakazi wa eneo hilo na maswali tele akilini mwao.

Wengi wa mabawabu hao walikuwa na miaka sitini na zaidi na walikuwa wanalinda maduka hayo,wauaji hao hawakuweza kuiba chochote licha ya kuvunja maduka hayo.

Bizarre case of the senseless killing of five watchmen in a night at Kilingili, Vihiga

Eneo hilo liko sasa katika vitabu vya polisi huku wananchi na wakazi wa eneo hilo wa salia na maswali kwanini polisi waliokuwa wakifanya usiku hawakuja kuwaokoa mabawabu hao.

Wana salia na maswali kwa maana kituo cha polisi kiko karibu sana na mahali mabawabu hao waliweza kuuwawa.

Baada ya kufanya unyama huo wauaji hao waliweza pia kuenda katika eneo la Ilungu na kisha kuwaumiza mabawabu wawili kisha kuenda.

Familia ya bawabu mmoja aliyefahamika kama Thomas Lusiolo walisema kuwa,aliweza kuwaambia kuwa aliweza kutishiwa maisha katika eneo hilo la kazi.

“Baba yangu aliweza kufanya kazi ya ulinzi Kilingili kwa zaidi ya miaka kumi,Jumanne aliweza kupokea vitisho vya maisha,

“Aliweza pia kumfahamisha tajiri yake kuwa ameweza kupokea vitisho,kisa ambacho pia kiliweza kujitudia Ijumaa,” Alisema Jane Minao msichana wake Lusiolo.

Mabawabu wale wengine ni pamoja na Linus Anyika,68, Francis Jojo,65, John Ondachi, 63, Charles Kalume, 60, aliyefariki akiwa katika hospitali ya Mbale.

Kamanda wa kaunti hiyo ya Vihiga Hassan Barua aliweza kuhakikisha mauaji hayo huku wakazi wakiwashtumu polisi kwa kulala wakiwa kazi.

Naibu wa gavana kaunti ya Vihiga Patrick Saisi aliweza kusimulia kitendo hicho kama cha unyama na kisichokuwa na huruma wowote.

“Nimeweza kuja mahala hapa kuhakikisha kama niliyoyasikia ni ukweli lakini nimepata ni unyama,ilhali tuko na kituo cha polisi hapa karibu,

“Nitaweza kupatana na mkuu wa polisi wa eneo hili ili niweze kumueleza na kufanya ombi,

“Kituo cha polisi kiko mita 50 na eneo la kisa hiki,lakini watu wetu wameweza kuuwawa,nataka polisi wa kituo hicho waweze kubadilishwa,” Alizungumza Patrick.