Monday, 22 June 2026
Kenyan Digest

Macron ashinda duru ya pili ya uchaguzi wa urais – Taifa Leo

Staff
1 min read
Published 26 April 2022

Macron ashinda duru ya pili ya uchaguzi wa urais

NA MASHIRIKA

PARIS, UFARANSA

RAIS Emmanuel Macron wa Ufaransa ataanza kuhudumu kwa kipindi cha pili kama rais, baada ya kutangazwa mshindi kwenye duru ya pili ya uchaguzi wa urais uliofanyika Jumapili.

Macron aliibuka mshindi kwa kuzoa asilimia 58.6 ya kura dhidi ya Marine Le Pen.

Wafuasi wake walishangilia ushindi huo kwenye barabara za jiji kuu, Paris, kati ya miji mingine.

Kwenye hotuba yake ya ushindi, aliahidi kurejesha tena hali ya mshikamano nchini humo.


About the author