Connect with us

General News

Maharagwe ndio yalitukosanisha na mke wangu

Published

on


Bwana Kipsang, 28, aliomba apatanishwe na mkewe bi Sharon ambaye anakiri aliamka siku moja na kusema kuwa amechoshwa na ndoa na kufunganya virago vyako na kuondoka.

Isitoshe Sharon aliondoka na mtoto wao mchanga.

“Unajua nilikuwa nimeoa kwa miaka mitatu na tarehe kumi na tano Januari aliniondokea bila tu kunijulisha baada yangu kwenda shughuli zangu, nilipompigia simu akaniambia eti ameenda kutafuta maisha.” Alieleza Kipsang.

Nikamuuliza nimemkosea wapi akaniambia sijamkosea lakini ameshindwa tu mpaka akaamua ajiendee. Mwenyewe nimebaki lonely hata nashindwa nifanye nini.

Nimejaribu kuongea na watu wa kwao mpaka nimefika huko, wakasema hawana habari yoyote na hata hawajajulishwa ameenda wapi.” Aliongeza akisema mkewe alimtumia ujumbe akisema kuwa tayari amefanikiwa na mume mwingine.

Sharon, 26, alipopigiwa simu alisema kuwa amekuwa akipitia mateso mikononi mwa Kipsang kwani bwanake alikuwa akimtesa mtoto aliyemua naye.

“Kipsang alinioa mwaka wa 2016 na akanioa nikiwa na mtoto na alikuwa na tabia ya kumtesa mtoto wangu, hata mtoto akiwa mgonjwa nikimwambia amshughulikie ananiambia nimpigie babake mtoto.” Alisema Sharon.

Mwezi wa nane last year aliuza maharagwe yote na hakunibakishia ya kutumia kwa nyumba, kumuuliza inakuwa ugomvi na maneno mengi tu kwa nyumba. Hata huyo mtoto mdogo alisema kuwa si wake hadi ikafika mahali nikakubali sio wake. Hakuwa anamshughulikia na isitoshe alikuwa anauza kila kitu hadi kuni!” Aliongeza Sharon.

Pata uhondo kamili.

 

 

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending