Wednesday, 10 June 2026
Kenyan Digest

Mashabiki waliopokea chanjo na ambao hawana virusi ndio wa pekee watakaohudhuria fainali za AFCON nchini Cameroon – Taifa Leo

Staff
1 min read
Published 17 December 2021

Mashabiki waliopokea chanjo na ambao hawana virusi ndio wa pekee watakaohudhuria fainali za AFCON nchini Cameroon

Na MASHIRIKA

MASHABIKI watakaoruhusiwa kuingia uwanjani kutazama mechi za fainali za Kombe la Afrika (AFCON) kati ya Januari na Februari 2022 nchini Cameroon ni wale watakaokuwa wamepokea dozi zote mbili za chanjo dhidi ya corona na watakaoonyesha vipimo vya kubainisha hawana virusi vya homa hiyo kali.

Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa na Shirikisho la Soka la Cameroon (Fecafoot) na Shirikisho la Soka la bara Afrika (CAF), fainali za AFCON zitafanyika kati ya Januari 9 na Februari 6, 2022.

Jumla ya timu 24, baadhi zikijivunia huduma za masupastaa wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kama vile Mohamed Salah wa Misri, Sadio Mane wa Senegal na Riyad Mahrez wa Algeria, zitashiriki.

Kipute cha AFCON kimecheleweshwa kwa muda wa mwaka mmoja kwa sababu ya janga la corona. Fainali za mwaka huu zitaandaliwa katika majiji matano tofauti ya Cameroon likiwemo jiji kuu la Yaounde.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO


About the author