Mbunge ahimiza wazazi wajitahidi kulipa karo shuleni
Na ALEX KALAMA
MBUNGE wa Kaloleni, Bw Paul Katana, amewaomba wazazi wajitahidi kulipia wana wao karo za shule, licha ya kuathiriwa kiuchumi na janga la corona.
Akizungumza na wanahabari katika wadi ya Mwanamwinga, alisema wale waliolemewa wazungumze na walimu kuhusu jinsi watakamilisha karo lakini wasitelekeze wajibu wao wa kulipa karo.“Tangu ugonjwa huu wa Covid-19 ulipoibuka, hakuna mzazi ambaye hajaathirika kiuchumi, lakini kwa heshima na taadhima nawaomba wale wazazi ambao watoto wao wako kidato cha nne, jitahidini mumalize kulipa madeni.
Zungumzeni na walimu vizuri lakini kusiwe na vikwazo bali muweze kuelewana nao ili watoto wasome,’ alisema Bw Katana.Kauli yake iliungwa mkono na diwani wa wadi ya Mwanamwinga, Bw Pascal Makanga, aliyedai kuwa visa vya wanafunzi kurejeshwa nyumbani kwa sababu ya karo vimekithiri eneo hilo.
Next article


