Wednesday, 10 June 2026
Kenyan Digest

Mchujo UDA wazua hofu tele Pwani – Taifa Leo

Staff
3 min read
Published 28 March 2022

Mchujo UDA wazua hofu tele Pwani

BRIAN OCHARO NA WACHIRA MWANGI

NAIBU Rais William Ruto, amelazimika kuingilia kati wasiwasi kuhusu mapendeleo katika kura ya mchujo wa Chama cha United Democratic Alliance (UDA) maeneo ya Pwani.

Katika ukanda wa Pwani, wanachama kadha walihama chama hicho miezi iliyopita wakisema uamuzi tayari ushafanywa kuhusu watakaowania viti kukipitia, hasa kwa wadhifa wa ugavana.

Hii ni baada ya Dkt Ruto kuonyesha wazi ukaribu wake na aliyekuwa seneta wa Mombasa, Bw Hassan Omar, Naibu Gavana wa Kwale, Bi Fatuma Achani, na aliyekuwa Gavana wa Taita Taveta, Bw John Mruttu, ambao wanataka ugavana katika kaunti zao.

Chama hicho kinatarajia kufanya kura za mchujo nchini kote mnamo Aprili 14. Kando na hayo, suala jingine lililoibuka majuzi kuhusiana na mchujo wa UDA Pwani ni kuhusu orodha ambayo inafaa kutumiwa kuamua watu wanaostahili kupiga kura.

Wiki iliyopita, maafisa wa bodi ya uchaguzi katika UDA walifanya mkutano na wajumbe wa chama hicho kutoka kaunti za Pwani mjini Kilifi ambapo ilibainika haku – na maelewano kuhusu orodha inayofaa kutumiwa katika mchujo.

Wajumbe waliohudhuria mkutano huo, akiwemo Mbunge wa Malindi, Bi Aisha Jumwa, walitaka orodha ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) itumiwe kuruhusu watu kupiga kura badala ya orodha ya wanachama wa UDA pekee.

Hata hivyo, maafisa wa chama waliokuwepo walisema uamuzi utatolewa baada ya mashauriano zaidi kufanywa.

“Kuna wale wana wasiwasi kwamba huenda wanachama wa UDA wamesajiliwa katika vyama vingine bila wao kujua kwa hivyo haitakuwa haki kuwafungia nje kuchagua viongozi wanaowataka,” alisema Bi Salome Beacco, afisa wa bodi ya kitaifa ya uchaguzi katika UDA.

Dkt Ruto jana alikutana na wanasiasa wanaotafuta tikiti ya chama hicho kuwania viti tofauti mjini Mombasa ili kuwaondolea hofu kuhusu kura ya mchujo.

Mkutano huo uliofanywa faraghani ulihudhuriwa na wanaotaka tikiti ya chama hicho, pamoja na viongozi wengine wa chama.

Mkutano mwingine kama huo ulipangiwa kufanyika katika Kaunti ya Kilifi baadaye mchana, kabla aelekee Malindi kwa mkutano wa hadhara.

Duru ziliambia Taifa Leo kwamba, suala lililopewa kipaumbele katika mkutano huo lilihusu kura ya mchujo ambapo wanasiasa walitaka hakikisho kutoka kwa Dkt Ruto kuwa zoezi hilo litafanywa kwa njia huru na ya haki.

Licha ya chama hicho kutangaza mara kwa mara kuwa mchujo utafanywa kwa njia ya haki, baadhi ya wanachama wamekuwa wakilalamikia uwezekano wa mapendeleo.

Dkt Ruto alianza ziara yake ya Pwani Jumamosi, ambapo alidai kuwa pesa zilizonuiwa kutekeleza miradi mikuu ya maendeleo katika Serikali ya Jubilee sasa zinatumiwa kufadhili siasa.

Alidai kuwa, Chama cha Jubilee kinachoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta, kinatumia pesa za umma kushawishi wanasiasa kujiunga nacho ili wapewe tikiti ya moja kwa moja kuwania viti katika uchaguzi ujao.

“Badala ya kuwapa watu wanaokufa njaa chakula, wanatumia pesa za serikali kununua wanasiasa. Hawa watu wanajua njaa kweli?” akasema, alipokuwa katika mkutano wa hadhara Mwembe Tayari.

Aliwakashifu wapinzani wake katika Muungano wa Azimio la Umoja akidai hawana ajenda ya kuboresha maisha ya wananchi.

Muungano huo unaongozwa na Rais Kenyatta, kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga, kinara wa Wip – er, Bw Kalonzo Musyoka, mwenzake wa Narc-Kenya, Bi Martha Karua, Mwenyekiti wa KANU, Bw Gideon Moi, miongoni mwa wengine.

Dkt Ruto anakumbwa na changamoto ya kushawishi jamii za Pwani jinsi atarekebisha athari za biashara zilizosababishwa na amri ya kutaka mizigo isafirishwe kwa reli ya SGR ku – toka Mombasa.

“SGR ambayo tulijenga kwa gharama kubwa haikunuiwa kuletea wakazi wa Pwani umaskini. Ilinuiwa kusaidia kuboresha uchumi na maisha ya wananchi,” akasema.

Canada waingia fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza...


About the author