Wednesday, 10 June 2026
Kenyan Digest

Mnangagwa aachia naibu wake mamlaka akianza likizo ya siku 23 – Taifa Leo

Staff
1 min read
Published 15 January 2022

Mnangagwa aachia naibu wake mamlaka akianza likizo ya siku 23

Na MASHIRIKA

HARARE, ZIMBABWE

RAIS wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amemkabidhi makamu wake mamlaka ya kuendesha nchi kwa siku 23 huku akienda likizoni.

Mnangagwa alianza likizo yake Ijumaa na atarejelea mamlaka yake Februari 5, 2022.

Naibu wa Rais Constantine Chiwenga ambaye pia ni Waziri wa Afya, ataendesha nchi kwa muda huo ambao Rais Mnangagwa atakuwa likizoni.

“Wakati huo ambao Rais atakuwa likizoni makamu wa rais Chiwenga atakuwa kaimu rais,” ikasema taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Rais na Baraza la Mawaziri Misheck Sibanda.


About the author